Eddy
alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia
darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka
kumwambia kitu muhimu....
Endelea...
Doreen
alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili
sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy..
Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi
kuziteka hisia za Eddy haswa.
Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
"Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.
"Naam"
"niambie basi.."
"ah!..
Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka
uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya
chini ili majirani wasiweze kusikia.
"Eddy!
we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen
alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata
Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa
Dorice.
"Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "
"Na Dorice je?"
"habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"
"mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.
"Nikubalie
Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi
yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen
alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.
"Okey! nakubali kuwa na wewe!"
"Oh
my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu
mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani
walikuwa darasani.
"Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."
"sharti gani tena?" Eddy alishtuka
"upo tayari?"
"ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"
"good.. nafurahi sana"
"Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.
"usijali nitakuambia baadae..."
Alisema
Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha
sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara
aliachia tabasamu.
Ilikuwa
ni mchana majira ya SAA nane na nusu ambapo kengele iligongwa katika
shule ya sekondari Mabango ambapo iliwaataarifu wanafunzi wote kuwa muda
wa vipindi umekwisha na ni muda wa kupata chakula cha mchana.
Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.
Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.
"Mkuu
wa shule mama Dayana Mbeshi ameaga dunia Leo asubuhi kwa kifo cha
ghafla kilichompata ofisini kwake..pia walimu wawili wana hali mbaya na
wamefikishwa hospitalini kwa matibabu!" ilikuwa sauti ya masikitiko sana
kutoka kwa Mwalimu Gallus iliyoonesha simanzi nzito sana aliyokuwa
nayo.
Mwalimu
huyo alishusha pumzi ndefu sana na kuendelea " Maombi yenu in muhimu
sana kwa walimu wenu ambao wapo hospitali... na..." mwalimu Gallus alishindwa kuendelea kuzungumza kwani machozi yalikosa adabu yakashuka kwa kasi hivyo akaamua kuondoka eneo lile.
Wanafunzi
wote waliondoka lakini mwishoni alibaki Eddy alitembea taratibu huku
picha ya msichana katili anayejifanya mwema, Doreen ikizidi kumjia
akilini mwake na kumfanya aisahau kabisa njaa aliokuwa nayo. Njia nzima
alkuwa akizungumza peke yake kama mwehu mpaka alipofika bwenini.
"Ah
Doreen! ni msichana mzuri sana! siamini kama amekuwa wangu..!" Aliwaza
Eddy huku akiachia tabasamu kisha akabadili nguo na kujitupa kitandani.
Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.
Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.
*******
Dorice
alikuwa amekaa kitandani kwake huku machozi yakitiririka mashavuni
mwake. Weupe wa ngozi ya USO wake ulibadilika na kuwa mwekundu kutokana
na kulia kwa muda mrefu, hakuamini kama Eddy angemtenda kiasi kiasi
kwani siku zote aliamini Eddy ndiye MTU pekee wa kumuamini, aliamini
kama Eddy ndio furaha pekee ya moyo wake iweje Leo amtupe kama taka ya
msafiri ndani ya basi pale airushapo kupitia dirisha bila kujua
itakapotua? Alimuona Eddy kama mnyama katili asiyekuwa na moyo wa utu.
Marafiki zake Dorice walizidi kumbembeleza atulie bila mafanikio yoyote.
"Kwa alichonifanyia Doreen, siwezi kumwacha kilahisi tu... lazima nimfanyie kitu..." Alijiapiza Dorice
"
Ni lazima atajuta mpaka kifo chake... hatokaa anisahau kwa
ntakachomfanyia.. lazima aelewe kuwa Mimi ni Dorice mtoto wa Kinyaturu
sinyang'anywi tonge mdomoni kwa urahisi!" Alizidi kujiapiza Dorice akiwa
amejifunika blanket mpaka usoni. Lakini baada ya muda mfupi Dorice
aliinuka kitandani pale na kujifuta machozi kisha akapiga hatua za
haraka kuelekea nje.
********
Mke wa Mwalimu John amuijia
Juu Mumewe akitaka kujua suruali ile imetoka wapi. Lakini mwalimu John
hakutaka kuweka wazi kile kilichomkumba shuleni.. alitaka iwe siri yake
mpaka atakapofanikiwa kwenda Malawi kutafuta waganga wakumroga
aliyemfanyia uchuro.
"John! umefumaniwa huko sio?" alifoka mke wa John
"usipaniki
mke wangu tulia.. sijafumaniwa mim!" alijitetea mwalimu John bila
mafanikio na wakati huo tayari mkewe alishaanza kumtandika makofi mumewe
na alipoona haitoshi akanyanyua upawa na kumtandika nao Mwalimu John
kichwani.
Ghafla John akanyong'onyea na kutulia kimya kitini bila kutikisika..
"John! John!" aliita mke wa mwlm John bila mafanikio John hakuweza kuitikia.
"Mime wangu... John wangu" alizidi kuita lakinu John alikuwa kimya, mkewe alichanganyikiwa sana.............