test
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Saturday, May 26, 2018

Mo Salah atacheza World Cup? Daktari wa timu atoa neno hili.

Mtanange wa yule Bingwa wa Ulaya umekamilika. Real Madrid wameshinda taji lao la tatu mfululizo kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Golikipa wa Liverpool Karius akisababisha uzembe ulioigharimu timu hao baada ya kurusha mpira kimakosa na ukagomga Benzema aliyegfunga bao la kwanza kabla ya Mane kusawazisha. unga magoli mawili. Bale alitokea benchi na kufunga mabao mawili.

Niliwahi kusema kinyago cha Gazzaniga (Kombe la Dunia) kiliwanyima mastaa wengi usingizi. Majeraha ilikuwa changamoto kubwa sana kwa wachezaji wa pande zote.
kilichotokea leo ni kitu ambacho wengi tulitarajia kutapoteza ladha ya mchezo huu.

Mo Salah ambaye alikuwa mchezaji tegemezi wa Liverpool hivi leo atolewa kwenye mchezo mapema kabisa baada ya kuumia bega. Ilikuwa ni kashkash kati yake yeye na Sergio Ramos. Ramos alikwenda kumkaba Salah na ilionekana wakishikana mkono. Picha na video zinaonesha kuwa alimvuta mkono na kumsababisha Salah kuondoka vibaya na kulalia bega lake.

Je wachambuzi wakubwa wanasemaje?
Rio Ferdinand
Ramos amekaba vyema. Alifanya kitu ambacho mlinzi yeyote angefanya. Sidhani kama alidhamiria.
Frank Lampard
mnapokuwa mmesogeleana sana mara nyingi ni rahisi sana kushikana mikono. ile ni bahati mbaya sana.

Rio na Lampard hawa ni waingereza na wana haki ya kutoa Maoni yao. Jana nilimsikia David Beckham aliweka pembeni sana suala la Uzalendo. Na aliweka mapenzi yake dhahiri kuwa Real inafaa iifunge Liverpool. Rio nae ni hasimu mkubwa wa Liverpool. Bila shaka ukiangalia ile video utagundua hakuna ajali. kuna tofauti kubwa ya kushikana na kumvuta mtu kwa makusudi ukidhamiria.

John Simpson anasema hivi
Nimeangalia maoni ya wachambuzi wakubwa, wanasema lile tukio ni ajali. Sawa. Lakini ukimwangalia Ramos wakati Salah anatolewa nje utagundua alidhamiria.

kuna baadhi ya video zinamuonesha Ramos akitabasamu na Mwamuzi wa pembeni.
David Maddock anasema
Inauma sana. Ramos amefanya kitendo cha kikatili haswa. Hajaharibu tu ndoto za Salah za Uefa pia huenda ameharibu ndoto wa Wamisiri wote.

Mo Salah taarifa zinasema mishipa ya bega imeachana. Na majibu kamili yatatolewa wakirudi jijini Liverpool. Hii inaleta wasiwasi mkubwa kama atahitaji kufanyiwa upasuaji. na itamlazimu kukosa michuano ya kombe la dunia.

hata hivyo taarifa za hivi punde zinasema kuwa ukurasa wa timu ya taifa ya Misri umeweka taarifa kuwa Mo Salah atacheza michuano ya kombe la dunia

Monday, May 21, 2018

Wambura analipwa Mil.7.....Kasema watia saini TFF walighushiwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura (49) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anapokea mshahara wa Shilingi Milioni 7 kwa mwezi.

Wambura ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, aiyekuwa rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Akiongozwa na wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza kutoa ushahidi wake, Wambura amebainisha kuwa aliwahi kuwasilisha maombi ya kutaka kuongezwa mshahara kutoka Shilingi Milioni 2 hadi 7 wakati wa utawala wa Malinzi.

Alipoulizwa na wakili Rweyongeza kwamba Malinzi alikataa kumuongeza mshahara, Wambura alidai kuwa si kweli, lakini alipeleka maombi hayo tena wakati wa utawala wa Rais wa sasa wa TFF, Walles Karia ambapo ameidhinisha alipwe Shilingi Milioni 7 tangu August 2017 hadi sasa.

Awali akiongozwa na Wakili wa serikali, Shadrack Kimaro, Wambura alidai kuwa muhtasari wa June 5,2016 uliokuwa na ajenda ya kubadilisha watia saini wa akaunti za Benki za TFF zilizopo Stanbic ni wa kughushi na kwamba yeye haufahamu.

Wambura amedai anasema hayo kwa sababu alikuwepo katika kikao hicho cha June 5,2016 na hakukuwepo na ajenda ya kubadilisha watia saini wa benki wa TFF kwa kumtoa Edgar Masoud na kumuingiza Nsiande Mwanga.

Baada ya kueleza hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi May 28 na 29 , 2018 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga. Pia Meneja wa Ofisi wa (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya.

Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 30 ikiwemo kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh 43,100,000.

Friday, May 18, 2018

Simba na Yanga zimepewa mchongo kucheza England

Kampuni ya SportPesa imeandaa mashindano ya timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambayo yanadhaminiwa na kampuni hiyo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Mashindano hayo yatafanyika Nairobi Kenya ambapo mshindi wa mashindano hayo atakwenda England kucheza na  moja ya timu ambazo zinadhaminiwa na kampuni hiyo.
Kwa upande wa Tanzania timu zitakazoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mapema mwezi Juni 2018 ni Yanga, Simba, Singida United pamoja na JKU ya Zanzibar.
“Mashindano hayo yalianza hapa (Tanzania) mwaka jana na sasa yanakwenda Kenya kwa mtazamo uleule na mafanikio yaleyale yaliyopatikana mwaka jana lakini safari hii mafanikio yatakuwa makubwa sana kwa sababu mshindi wa mashindano haya anaweza kwenda kucheza Uingereza”-Abbas Tarimba, mwakilishi wa SportPesa Tanzania.
“Mshindi atakaekwenda kucheza Uingereza atanufaika si tu na dakika 90 za mchezo lakini kuna mambo mengi ambayo wanaweza kujifunza ikiwa ni pamoja na kuendeleza weledi wao katika mpira wa miguu.”
“Mashindano yatashirikisha timu nane, nne kutoka Kenya na nne kutoka Tanzania hivyo ni mashindano yenye chachu kubwa sana na yanafanyika wakati mzuri sana.”

Wednesday, May 16, 2018

Rais Magufuli Akubali Kuikabidhi Kombe Simba SC

Shirikisho la soka nchini TFF leo Mei 16, limethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi na kukabidhi vikombe vya ubingwa wa Serengeti Boys na Simba.

Mtendaji mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema wamethibitishiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Rais Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar jumamosi hii.

''Rais Magufuli amekubali ombi la TFF kuwakabidhi vijana wa Serengeti Boys Kombe la CECAFA waliloshinda hivi karibuni nchini Burundi, tukio ambalo litaambatana pia na kuikabidhi Simba SC kombe la ubingwa wa VPL msimu huu'',  amesema.

Serengeti Boys wameibuka mabingwa wa soka katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuwafunga vijana wa Somalia kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.

Simba imetwaa ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18 baada ya kufikisha alama 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya 16 za ligi kuu msimu huu.

Monday, May 14, 2018

Tanzania yatinga hatua ya fainali kombe la Dunia

Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoundwa na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa Kituo cha TSC Mwanza wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu baada ya kuifunga Uingereza magoli 2-1.

Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la klabu ya Lokomotive mjini Moscow nchini Urusi Tanzania iliibuka na ushindi huo mnono kupitia kwa wachezaji wake, Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari.

Kwa upande mwingine timu ya Brazili imetinga hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya  Ufilipino.

Tanzania ambayo ndiyo mabingwa watetezi baada ya kulitwaa kombe hilo mwaka 2014, itaikabili Brazil kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kupigwa kesho kutwa huku mpaka sasa ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.

Thursday, May 10, 2018

Yanga Yaipigia Saluti Simba “Kwa Hali Ilivyo Simba Ndiyo Mabingwa"

Yanga Yaipigia Saluti Simba “Kwa Hali Ilivyo  Simba Ndiyo Mabingwa"
HATIMAYE benchi la ufundi la Klabu ya Yanga limeamua kukubali kuwa wapinzani wao Simba kwa msimu huu ndiyo mabingwa huku wao sasa wakijipanga kuelekeza nguvu zao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.



Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu baada ya kuutwaa msimu uliopita wakiwazidi Simba kwa mabao ya kufunga lakini kwa msimu huu hadi sasa wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 48 ambazo ni pointi 17 nyuma ya Simba wanaongoza ligi wakiwa na pointi 65.



Akizungumza na Championi Jumatano, muda mfupi baada ya kurejea kutoka nchini Algeruia, Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Zahera Mwinyi alisema kwa sasa wamekubali kuwa wapinzani wao ndiyo mabingwa wa ligi huku wao wakielekeza nguvu sasa katika michuano ya kimataifa ambayo wanashiriki.



“Kwa hali ilivyo kwa sasa Simba ndiyo mabingwa wa ligi kwa msimu huu huku sisi tumepanga kwa sasa kuelekea nguvu zetu katika michuano ya kimataifa ambapo tunashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.


“Tunaelekeza nguvu huko kwa sababu hapa Tanzania hatuwezi kuwa mabingwa lakini pia Kombe la FA tumeshatolewa,” alisema Zahera.

Akizungumzia juu ya mwanzo mbaya wa kikosi hicho katika mchezo wake wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Mkongomani huyo alisema:



“Tulienda na wachezaji ambao hawana uzofu na michuano hii na ndiyo sababu iliyochangia kwetu kufungwa mabao 4-0 mbele ya wapinzani wetu, licha ya kwamba walifuata maelekezo ya kile ambacho niliwaambia.



“Wachezaji wale muhimu tuliwaacha hapa Dar, utaona jinsi jambo hilo lilivyoweza kuchangia sisi kupoteza mechi yetu ya huko. Nimepanga kuongea na uongozi ikiwezekana kwamba kuwe na timu mbili ambapo moja itaenda Mbeya kucheza na Mbeya City (kesho Alhamisi) halafu ikimaliza iende pia Morogoro kucheza na Mtibwa.



“Wakati huohuo pia kuwe na timu ambayo nitabaki nayo hapa Dar ambayo itajumuisha wale wachezaji ambao hawakwenda Algeria ambao nitakaa nao na kuzungumza, hii timu nitawapa mafunzo kuhakikisha kwamba inafanya vyema kwenye mchezo wetu dhidi ya Rayon Sport.



“Nafanya hivyo kwa sababu nataka nguvu zetu nyingi tuelekeze huko kwenye michuano ya kimataifa kwani ndiyo nafasi pekee ambayo imebaki kwetu kuona tunashiriki michuano ya Afrika kwa msimu ujao, kwani hakuna sehemu nyingine zaidi ya huku hivyo yatupasa kuweka nguvu zaidi,” alisema Mkongomani huyo.

Friday, May 4, 2018

Manara apewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu, aomba radhi

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amepewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.

Manara amepewa barua iliyomuonya kutokana na kukiuka sheria za michezo za ligi kuu mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Mtendaji Mkuu wa Bodi Ligi, Boniface Wambura ameeleza kuwa uamuzi huo umeafikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichopitia taarifa na matukio mbalimbali ya ligi msimu wa 2017/18 yanayoendelea kulindima hivi sasa, ambapo kilibaini tukio la utovu wa kinidhamu kwa afisa huyo.

“Katika mechi namba 178 dhidi ya Yanga SC iliyochezwa Aprili 29, 2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa aliingia uwanjani Haji Manara kushangilia ushindi wa timu yake. Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo, inayozuia wasiohusika kuingia uwanjani kabla, baada na wakati mechi ikiendelea”, amesema Wambura.

Kwa upande wake, Haji Manara ameonesha kulitambua kosa lake na kuiomba radhi Bodi ya Ligi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), pamoja na wadau wote wa soka, huku akieleza kuwa furaha ndiyo iliyompelekea yeye kutenda kosa hilo.

“Muungwana akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa mshabiki kama kumgalagaza mtani…it will never happen again..ila sijui itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwali😁😁😁 @tanfootball #bodiyaligi 🙏🙏” ameandika Haji Manara karika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Katika Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa namashabiki wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini, Simba iliibuka kidedea baada ya kuichapa Yanga goli 1 ambalo lilifungwa dakika ya 37 na Erasto Nyoni.

Tuesday, July 12, 2016

UEFA wametaja kikosi bora cha michuano ya Euro 2016

Siku moja baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika na timu ya taifa ya Ureno kutwaa taji Kombe hilo, leo July 11 2016 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetaja majina ya wachezaji 11 bora wanaounda kikosi bora cha Euro 2016.
UEFA wametaja majina 11 ya wachezaji kutoka nchi za Ureno, Ufarasa, Ujerumani na Wales, kwa upande wa Ureno wametoa jumla ya wachezaji wanne, Ujerumani watatu, Ufaransa na Wales wawili wawili kila timu, lakini kama utakuwa unakumbuka Ronaldo bado ni mmoja kati ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha muda wote cha Euro.
tott

VIDEO: Jikumbushe TOP 5 ya magoli bora ya hatua ya mtoano Euro 2016



Monday, July 11, 2016

URENO YASHINDA KOMBE LA EURO 2016

FT (after Extra Time) PORTUGAL 1, FRANCE 0.

Eder's 1st international goal wins Portugal their 1st title. Incredible!

image.png

image.jpeg

image.jpeg

=====
UPDATES

Confirmed lineups

image.jpeg

ImageUploadedByJamiiForums1468173182.282925.jpg

01min: POR 0 - 0 FRA

10min: POR 0 - 0 FRA

16min: POR 0 - 0 FRA

30min: POR 0 - 0 FRA

40min: POR 0 - 0 FRA

HT: POR 0 - 0 FRA

Sunday, July 10, 2016

Sentensi za Mama yake Ronaldo Baada ya Kumuona Mwanae Analia


Usiku wa July 10 2016 mchezo wa fainali ya Euro 2016 ulichezwa na kushuhudia timu ya taifa ya Ureno ikifanikiwa kutwaa Kombe la Euro kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhid ya mwenyeji Ufaransa.

Tukio la kuumiza kwa mashabiki wa Ureno ni pale dakika ya 23 nahodha wao Cristiano Ronaldo alipotolewa nje ya uwanja kwa machela akiwa analia baada ya kushindwa kuendelea na mechi kutokana na kufanyiwa faulo mbaya.

Muda mfupi baada ya Ronaldo kutolewa analia, mama mzazi wa staa huyo Dolores Aveiro aliandika ujumbe wake kutumia account yake ya twitter unaoonesha kusikitishwa kwake kwa faulo aliyofanyiwa mwanae

Siwezi kumuangalia mwanangu akiwa katika hali hii (analia), huu mchezo ina maana kucheza mpira sio kumuumiza mpinzani”

VIDEO:Ureno Kutoka Best Loser Hadi Mabingwa wa UERO 2016


Ureno wameweza kuikabili Ufaransa na kuichapa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2016 na kushinda taji lao kubwa kwa mara ya kwanza bila ya nahodha wao Cristiano Ronaldo aliyetoka mapema kipindi cha kwanza baada ya kuumia. Loser

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid alibebwa kwenye stretcher huku akibubujikwa na machozi dakika ya 25 ya mchezo dakika nane baada ya kuumia goti alipopambana na mfaransa Dimitri Payet.

Ufaransa timu ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa huo, walishindwa kupata bao kwa kutumia faida ya kukosekana kwa Ronaldo uwanjani licha ya kukaribi kupata bao dakika za lala salama kupitia kwa Andre-Pierre Gignac aliyeingia kutoka benchi ambapo shuti lake liligonga mwamba.

Raphael Guerreiro alipiga mpira wa adhabu ndogo uliogonga mtambaa panya lakini sekunde chache baada ye Eder aliachia shuti la chinichini akiwa umbali wa mita 25 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Ufaransa Hugo Lloris na kuzama wavuni.

Ronaldo ambaye alikuwa akiwahamasisha wachezaji wenzake wakati wa mapumziko kabla ya dakika 30 za nyongeza, alikuwa akitekeleza majukumu ya benchi la ufundi sambamba na kocha Fernando Santos hasa wakati wa dakika za mwisho na alishindwa kuzuia machozi ya furaha baada ya filimbi ya mwisho kabla ya kunyanyua ndoo aliyoisubiri kwa muda mrefu akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno.

Matukio katika namba

35: Ureno wameshinda taji lao la kwanza la Ulaya baada ya mechi 35 kwenye mashindano hayo.

10: Ureno ni taifa la kumi tofauti kushinda kombe la mataifa ya Ulaya.

6: Eder ni mchezaji wa sita kufunga goli kwenye michuano ya Ulaya akitoea benchi anaungana na Oliver Bierhoff, Sylvain Wiltord, David Trezeguet, Juan Mata pamoja na Fernando Torres.

3: Ureno imekuwa nchi ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya kucheza mechi tatu hadi dakika 30 za nyongeza ndani ya msimu mmoja wa mashindano.

80: timu ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kupiga shuti lake on target dakika ya 80, muda mrefu zaidi kwenye fainali za michuano ya Ulaya.

Video ya highlights za mechi ya Ureno dhidi ya Ufaransa

EURO 2016: Fainali- Nani Atanyakua Kombe leo? Utabiri Na Mambo Yote Muhimu Unayohitaji Kuyafahamu

Euro 2016 Final-France Versus PortugalHatimaye michuano ya Euro 2016 (Kombe La Mataifa Ya Ulaya La Soka) iliyoanza tarehe 10 Juni 2016 inafikia ukingoni Jumapili hii tarehe 10 Julai, 2016 kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji Ufaransa dhidi ya Portugal (Ureno). Kwa saa za Afrika Mashariki kipyenga kitapulizwa mida ya saa nne usiku.
Refarii ambaye amepangwa kuchezesha mechi hii ni  muingereza Mark Clattenburg (41) anayechezesha English Premier League(EPL). Huyu ndio refa aliyechezesha pia fainali ya Kombe La Klabu Bingwa Ulaya (UEFA Champions League) kati ya Real Madrid na Atletico Madrid tarehe 28 Mei jijini Milan, Italy.
Vituo mbalimbali vya Televisheni na hususani DStv (MultiChoice) vitarusha matangazo ya moja kwa moja ya mpambano wa fainali. Mpambano huu utafanyikia jiji Paris katika viungwa vya Saint-Denis katika uwanja maarufu wa Stade De France. Huu ndio uwanja ulioshuhudia Ufaransa wakinyanyua Kombe La Dunia katika fainali za mwaka 1998 walipoichapa Brazil 3-0 katika mchezo wa fainali.
Kama unafuatilia masuala ya soka, bila shaka unakumbuka baadhi ya mechi, matukio na jinsi Ufaransa na Ureno zilivyoofikia hatua hii ya kilele cha michuano. Kama hukumbuki, naomba nikukumbushe kidogo.
Safari ya timu hizi mbili kufika hatua ya fainali haikufanana. Ufaransa wameingia fainali wakitokea Kundi A. Huko walishinda 2-1 dhidi ya Romania, wakashinda 2-0 dhidi ya Albania, wakaenda sare ya 0-0 dhidi ya Switzerland. Wakatinga hatua ya makundi. Katika hatua ya makundi waliifunga Ireland goli 2-1 na kutinga robo fainali ambapo waliifunga Iceland goli 5-2. Katika Nusu Fainali wakaifunga Ujerumani goli 2-0.

Mark Clattenburg-Refa atakayechezesha fainali ya Euro 2016 kati ya Ufaransa na Ureno
Mark Clattenburg-Refa atakayechezesha fainali ya Euro 2016 kati ya Ufaransa na Ureno
Kwa upande wa Portugal(Ureno) safari yao ilikuwa ya kusuasua. Mashabiki wengi wa soka hawaamini wala kuelewa wamefikaje fainali. Mimi ni mmojawapo. Lakini soka ni mchezo ambao, kama ilivyo kwenye michezo mingine, bahati inahusika japo kidogo.Naamini Portugal wana bahati. Mtaani tunaweza kusema zali lipo upande wao katika michuano ya mwaka huu.
Wao wamefika hapa wakitokea Kundi F. Walianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Iceland. Kisha wakatoka sare ya 0-0 dhidi ya Austria na kumaliza kwa sare ya 3-3 dhidi ya Hungary. Walimaliza wakiwa namba 3 kwenye kundi.
Katika hatua za makundi wakaifunga Croatia goli 1-0 kwa goli la Ricardo Quaresma katika dakika za nyongeza. Katika robo fainali wakakutana na Poland. Hadi dakika 120 ngoma ilikuwa 1-1. Mikwaju ya penati ikaamua mshindi. Portugal wakasonga mbele kwa penati 5-3. Katika mchezo wa nusu fainali walikutana na Wales. Wakajipatia ushindi wao wa kwanza wa ndani ya dakika 90 za kawaida kwa kuwalaza Wales 2-0.
Unaweza kuona kwamba kama isingekuwa utaratibu mpya wa UEFA wa kupeleka mashindanoni timu 24 badala ya 16, bila shaka Ureno wangeshasahau kama walishiriki. Kimkandamkanda wakaingia kama timu bora ya tatu. Lakini waswahili tunasema yaliyopita si ndwele. Wameshatua fainali.
Katika historia kuanzia mwaka 1975, Ufaransa wamekutana na Ureno zaidi ya mara kumi. Katika mipambano hiyo yote Ufaransa wameshinda. Hapo ni tangu Christiano Ronaldo hajazaliwa.
Stade De France-Uwanja utakapofanyikia mchezo wa fainali kati ya wenyeji Ufaransa dhidi ya Ureno
Stade De France-Uwanja utakapofanyikia mchezo wa fainali kati ya wenyeji Ufaransa dhidi ya Ureno
Kama historia ni jambo la kuaminika na kutegemewa basi Ufaransa wanayo nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa mwaka huu. Kwanini? Mbali ya kuwa wameshawageuza Ureno “vibonde” wao, historia inayonyesha kila wanapoandaa michuano mikubwa huishia kuwa mabingwa. Walipoandaa michuano kama hii mwaka 1984 waliibuka washindi. Walipoandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998, waliibuka mabingwa.
Kila mchezo huwa na nyota wake. Kwa Ufaransa na Ureno kuna wachezaji wawili ambao dunia itakuwa ikiwatazama. Wote wanacheza katika La Liga. Kwa upande wa Ureno, Christiano Ronaldo. Ufaransa wanaye Antoine Griezman anayechezea Atletico Madrid.
Mpaka sasa Antoine Griezman ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao akiwa na magoli 6. Christiano Ronaldo ana magoli 3. Hata hivyo Ronaldo ameweka rekodi ya kumfikia mfaransa Michél Platini kwa kuwa na idadi sawa ya magoli. Wote wana magoli 9 ambayo ni rekodi katika michuano hii ya Ulaya. Bila shaka Griezman atakuwa na hamu ya kuiongoza Ufaransa kwenye ubingwa na kuwa mshindani katika Ballon D’or. Christiano ambaye alishafika katika hatua hii mwaka 2004 na kupoteza dhidi ya Ugiriki atakuwa na hamu ya kuondoa lile balaa.
Mwezi Mei, Ronaldo na Griezman walikutana jijini Milan katika mpambano wa Real Madrid na Atletico Madrid. Hakuna aliyezifumania nyavu mpaka kwenye matuta. Ronaldo aliibuka na kicheko mwishoni. Real Madrid wakaibuka mabingwa. Hali ni tofauti nchini Ufaransa. Hawachezei vilabu.Wanapambana wakiwa na timu zao za taifa. Na Ufaransa watakuwa wakisindikizwa na mamilioni ya mashabiki wao.
Utabiri wangu ni kwamba Ufaransa itachukua Kombe. Nimewaunga mkono katika safari yao hii tangu mwanzo. Naamini advantage ya uwanja wa nyumbani ni kubwa. Sio rahisi waruhusu kombe liondoke. Lakini mpira ni dakika 90. Mpira unadunda. Lolote linaweza kutokea.

Friday, July 8, 2016

Ufaransa itapambana na Ureno katika Fainali za #EURO2016 baada ya kuinyuka


Thursday, July 7, 2016

BREAKING NEWS!! MESSI AHUKUMIWA KIFUNGO JELA.

Mchezaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti.
Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.
Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha.

Wednesday, June 8, 2016

England kick off their Euro 2016 campaign against Russia on Saturday but who should they play in attack?



1
Harry Kane
  
2
Jamie Vardy
  
3
Wayne Rooney
  
4
Marcus Rashford
  
5
Daniel Sturridge
  
6
Raheem Sterling

Friday, June 3, 2016

Confederation Cup: Nyanga FULL AGAINST THE BDF GADO TODAY.........!!!!



Nyanga is ready for anything! If you do not agree, today at 2:30 at night waiting to see at work against BDF XI.

Yanga requires uniform of any kind in order to move forward, or preferably victory, just cool too!

Yanga whole band mandalizi Done it for replay African Confederation Cup against the team of Botswana Defence Force, matches to be held in Lobatse Stadium, 70 kilometers from the city here.




Man Uniteds Jose Mourinho has a family outing at Wembley to watch England 1 Portugal 0 [Instagram] Mourinho watches England v Portugal

Man Uniteds Jose Mourinho has a family outing at Wembley to watch England 1   Portugal 0 [Instagram]
Jose Mourinho may be a newcomer to Instagram, but he clearly knows how to use the platform.
The Man United boss uploaded a new image to his social media account on Thursday night revealing how he was in attendance at Wembley.
The Special One enjoyed a family outing, as he watched England warm up for Euro 2016 with a 1-0 win over his home nation, Portugal.
Man United defender Chris Smalling is sure to have impressed his onlooking manager, as the centre-half scored a late winner to seal a third straight win for the Three Lions.

Monday, May 30, 2016

Real Madrid Beat Atletico Madrid On Penalties to win the Champions League

Real Madrid have won the Champions League for the 11th time, beating Atlético Madrid 5-3 on penalties, with Cristiano Ronaldo hitting the winning spot-kick after a 1-1 draw.
After successful kicks for Real by Lucas Vázquez, Marcelo, Gareth Bale and Sergio Ramos, and for Atlético by Antoine Griezmann, Gabi and Saúl, Juanfran’s penalty was saved and Ronaldo did the rest
Real took the lead in the 15th minute when Sergio Ramos turned the ball in from close range after Bale flicked on a Toni Kroos free-kick.
Atlético were awarded a penalty early in the second half, after Torres cleverly got across Pepe, let the ball run past him and the defender bundled into him. But Griezmann’s effort rebounded off the crossbar.
However, with 11 minutes left, shortly after Bale had an effort cleared of the line, Griezmann lofted a ball down the right channel for Juanfran, who volleyed across goal to find Yannick Carrasco, who smashed it home.
Neither side was able to score again in either normal time or the extra half-hour, and the second all-Madrid final – two years after Real won the first – went to spot-kicks.

Friday, May 27, 2016

Man United has officially announced to give Jose Mourinho a contract

Top Management of Man United today May 27 2016 has officially announced to give Jose a contract of three years to a former coach of Chelsea Jose Mourinho with the feature remain at the club until 2020.

Jose Mourinho has been announced by the club but will join and start working officially 2016/2017 season this year means we will begin to see Mourinho leading Man United as head coach during a match of preparation for the match of the season.

As you will recall correctly Jose Mourinho was sacked by Chelsea December 2015, a natural coach of Portugal from 2003 until now as a coach he has won a total of 23 Shells in 4 different countries.
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU