ABIRIA
10 kati ya abiria 30 waliokuwa wakisafiri kwenye boti wakitokea
Mitomoni, wilaya ya Songea Vijinini, mkoani Ruvuma kwenda mnadani katika
wilaya hiyo wanahofiwa kufa maji baada ya boti hiyo kuzama kwenye Mto
Ruvuma.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa zilieza kuwa, boti hiyo ilikuwa
imejaza abiria pamoja na mizigo iliyokuwa ikipekwa kwenye mnada wa
hadhara ambao upo jirani na kijiji cha Mitomoni mpakani mwa Tanzania na
Msumbiji.
Jitihada za kumtafuta
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, hazikufanikiwa baada
ya kuelezwa kuwa alikuwa ameungana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Ruvuma kwenda kwenye eneo la tukio hilo.
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa
Ruvuma, Hamis Kutiku, alisema Kamanda Mwombeji amekwenda kwenye eneo la
tukio ili kujiridhisha ukweli wa tukio hilo.
Alisema taarifa
kamili juu ya tukio hilo zitatolewa baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama
kufika eneo la tukio na kurudi mjini kwa ajili ya hatua zaidi
kuchukuliwa.