test

Saturday, July 9, 2016

Khadija Kopa Adai Ngono Inawazeesha Wasichana Wengi

 Malkia wa mipasho Khadija Kopa amefunguka kwa kusema kuwa ngono ni moja kati ya vitu ambavyo vinawazeesha wasichana wengi.

Akiongea katika kipindi cha Ulimwengu wa Filamu kinachoruka TBC 1 Jumamosi hii, Khadija Kopa amesema yeye hazeeki kwa sababu siyo mtu wakuendekeza maswala ya ngono.

“Mimi najitunza sana ndo maana kila siku naonekana bado mbichi,” alisema Khadija. “Unajua wasichana wengi wanaendeleza maswala ngono, ngono inazeesha sana, haya makrimu ndo usiseme, ukiweza kukaa nayo mbali basi kila siku utaonekana mbichi,”

Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amewataka mashabiki wake wa muziki kusubiria kazi mpya ambazo ataziachia hivi karibuni.
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU