test

Sunday, July 31, 2016

KAHAMA KWA WAKA MOTO:Lembeli, Kuhama msikiti siyo kuacha Uislamu.



Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema ameibuka leo katika mkutano wa Rais John Magufuli uliofanyika mjini Kahama.
Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi  CCM akisema kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza mkia, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.
Akizungumza kwenye mkutano huo Lembeli amesema alikwenda kwenye mkutano huo kwa kuwa kazi anayofanya Rais Magufulli ndiyo aliyokuwa anapigania wakati akiwa Mbunge kwa kuwa Shinyanga rushwa iikuwa imezidi.

Amesema hawezi kurudi kwenye chama hicho mpaka Rais Magufuli akisafishe.
Kuhama msikiti siyo kuacha Uislamu,nyumba itakaposafishika nitarudi.Alisema Lembeli huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliokuja kumlaki Rais Magufuli.
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU