TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo inatarajiwa kuwapandisha kizimbani wafanyabiashara wawili akiwemo Mohamed Mustafa Yusufali ‘Choma’ aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh milioni saba kwa dakika moja kwa njia za udanganyifu katika mapato ya serikali.
Choma
na mfanyabiashara wa Arusha, Samweli Lema, walifikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana saa 9 mchana kwa ajili ya
kusomewa mashitaka yanayowakabili, lakini ilishindikana kwa sababu muda
ulikuwa umekwisha.
Washtakiwa
hao waliondolewa katika viwanja vya mahakama hiyo jioni na kurudishwa
mahabusu kwa kutumia magari ya Takukuru, hivyo leo wanatarajiwa
kupandishwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao.
Choma atakuwa anakabiliwa na kesi mbili
kwa wakati mmoja, kwa kuwa Julai 12 mwaka huu, alifikishwa mahakamani
hapo na wenzake wakikabiliwa na mashitaka 199 likiwemo la kuisababisha
serikali hasara ya Sh bilioni 15.6.
Awali
kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 inayomkabili
Choma na wenzake Alloyscius Gonzaga Mandago, Isaack Kasanga, Taherali
Sujjauddin Taherali na Mohamed Kabula ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu Huruma Shahidi.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa
kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya
kutajwa.
Aidha, aliiomba Mahakama iwaruhusu kumchukua Choma kwa ajili ya kumhoji kutokana na tuhuma mpya zinazomkabili na kuahidi kumrudisha mahakamani kabla saa za kazi hazijaisha.
Aidha, aliiomba Mahakama iwaruhusu kumchukua Choma kwa ajili ya kumhoji kutokana na tuhuma mpya zinazomkabili na kuahidi kumrudisha mahakamani kabla saa za kazi hazijaisha.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Shahidi alimuuliza mshtakiwa huyo kama ana
lolote la kusema, alikaa kimya lakini baadaye alidai kuwa ameelewa na
atakuwa tayari endapo wakili wake atakuwepo kwenye mahojiano hayo.
Hakimu Shahidi aliruhusu upande wa Jamhuri umchukue mshtakiwa huyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 5, mwaka huu.
Choma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Superior Financing Solution Limited kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Julai 12, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka 199 ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, uhujumu uchumi utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6.
Choma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Superior Financing Solution Limited kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Julai 12, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka 199 ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, uhujumu uchumi utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6.
Katika
mashitaka ya kughushi inadaiwa alighushi hati za usajili kuendesha
kampuni 15 ikiwemo Festive General Business Limited zimesajiliwa
kihalali nchini jambo ambalo si kweli. Aidha, anadaiwa kuwasilisha
nyaraka hizo za kughushi kwa Kamishna wa Kodi Ofisi za TRA Mkoa wa
Kinondoni ili kuonesha kampuni hizo zimesajiliwa na zinastahili
kusajiliwa kama mlipa kodi.
Mbali
na mashitaka hayo, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha fedha, kwa
kuficha uhalali, chanzo na mzunguko wa Sh 1,895,885,000 kwa kuzikopesha
fedha hizo kwa watu mbalimbali na kupokea marejesho ya mikopo huku
wakijua fedha hizo zimetokana na njia zisizo halali za kughushi na
kukwepa kodi.
Yusufali
anadaiwa kati ya Januari 2008 na Januari mwaka huu, kwa vitendo viovu
vya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Kamishna wa TRA,
ameisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 ambazo zilitakiwa
kulipwa kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).