test

Monday, July 11, 2016

Mtangazaji Gadner G Habash Afunguka Kuhusu Kuhamia Clouds FM Kutoka EFM...Adai Maslahi Manono Yalimwamisha


“Maisha ni mazuri sana, ni maisha kama ukurasa mpya ambao nimeufungua,” alisema Gadner. “Namshukuru sana sana Mwenyezi Mungu amenipa kipaji lakini nawashukuru zaidi management ya Clouds FM kuona kwamba ninafaa nirudi pale tushirikiane tena, kwangu mimi naona ni kitu kikubwa japokuwa nilifanya kazi na Clouds FM kwa miaka 9 lakini bado hii nimeiona kama ni ukurasa mpya na nikitu kipya na ndio maana unasikia nasound kama mtu mpya,” alisema Gadner.

Pia mtangazaji huyo alizungumzia aliwezaje kurudi tena Clouds FM wakati tayari alishaanza maisha mapya na vituo vingine vya redio kama EFM.

“Ilikuwa ni vigumu sana kuondoka pale nilipokuwa (EFM) kwa sababu ya mazoea na urafiki ambao tulikuwa nao baina yangu mimi pamoja na staff ambao nilifanya nao kazi, baina yangu pamoja na viongozi, lakini wakati mwingine unapofanya uwamuzi, unahitaji kutumia hekima sana ili ufanye uwamuzi bila kuwa na hisia za kibinafsi, ufanye uamuziki kutokana na nini biashara inataka, au ni nini maslahi yanataka na ndo utumie akili kuona kama maslahi yao. Zaidi ya hapo ujitahidi uondoke kwa mazingira yalio salama bila kukwazana na wale unaoachana nao, lakini ilikuwa ni ngumu, lakini kwa sababu Clouds FM walikuwa wananithamini kiukweli wamenipa offer ambayo ni kubwa sana na unajua wakati mwingine unamuomba mungu, lakini Mungu anakuletea bila kujua kama anakuletea nafikiri katika dua zangu ambazo nilimuomba Mungu aniongezee naona mkataba wangu mpya wa Clouds ameniongezea,”
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU