test

Friday, March 2, 2018

Wanafunzi 400 wavamia Nyumba ya Mwalimu na Kufanya Vurugu....Shule Yafungwa Wiki 2

Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo iliyoko Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya wanafunzi wake kuzusha vurugu kubwa huku wakivamia na kuivunja ofisi ya Makamu Mkuu wa shule hiyo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu, alithibitisha jana kuifunga sekondari hiyo ya kitaifa kuanzia Machi Mosi hadi Machi 17, mwaka huu.

Shule hiyo ya kitaifa hupokea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita kutoka mikoa mbalimbali nchini.

"Ni kweli nimeifunga hiyo shule kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na sababu za kiusalama. kulikuwa na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi na wakati unafanyika mwanafunzi mmoja aliandika matusi makubwa akiwatukana walimu.

"Baada ya kufanyika uchunguzi aligundulika huyo mwanafunzi na hapo ndiko walipoandaa vurugu hizo na kujielekeza kuharibu mali na kusababisha hasara ambayo bado haijafahamika," alisema Buswelu.

Kwa mujibu wa Buswelu, vurugu hizo ziliibuka baada ya mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) kupewa barua ya kufukuzwa shule kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Buswelu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha ameagiza Bodi ya shule hiyo kukutana kesho (leo) kufanya tathmini ya hali ya uharibifu na madhara yaliyojitokeza na kuiarifu serikali.

Mpaka sasa, hakuna mwanafunzi anayeshikiliwa kwa kufanya vurugu na kusababisha hasara ya mali na rasilimali za serikali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hamisi Issah, alisema wanafunzi hao walifanya tukio hilo saa 4:30 asiku juzi.

"Hao wanafunzi wameharibu ofisi ya mwalimu huyo ambaye pia ni mwalimu wa nidhamu kwa kuvunja paa la juu, milango, madirisha na samani za ndani," alisema Kamanda Issah.

Related Posts:

  • Wanawake 40 Kunyongwa Iraq Serikali inatarajia kuwanyonga wachumba 40 wa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) kulipiza kisasi kwa wapiganaji hao wa jihadi kuikalia kwa miaka mitatu ardhi ya Iraq wakati wa mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu k… Read More
  • Facebook Yaendelea Kuomba Msamaha Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwenye Bunge la Ulaya kutokana na madhara yaliyosababishwa na kuvuja kwa data za watumiaji wa mtandao huo na pia kwa kushindwa kupambana na habari za uongo/ feki. … Read More
  • Iran yaendelea kupinga masharti ya Marekani Iran imeendelea kupinga masharti kutoka Marekani ya kufanyia mabadiliko sera yake ya kigeni na mpango wake wa nyuklia huku mshirika wake Syria, ikitupilia mbali wito wa Marekani kuviondoa vikosi vya Iran nchini humo. … Read More
  • Mo Salah atacheza World Cup? Daktari wa timu atoa neno hili. Mtanange wa yule Bingwa wa Ulaya umekamilika. Real Madrid wameshinda taji lao la tatu mfululizo kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Golikipa wa Liverpool Karius akisababisha uzembe ulioigharimu timu hao baada ya kurush… Read More
  • Kim Jong-un azidi kumvuruga Trump Rais wa Marekani, Donald Trump ametilia shaka kuhusu kufanyika kwa mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un mwezi june mwaka huu huko Singapore. Ameyasema hayo mara baada ya Korea Kaskazini kutishia kujio… Read More

0 comments:

Post a Comment

TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU