Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amebainisha kuwa baba yake
ni moja kati askari kutoka Tanzania ambao wamepigana vita nyingi
kwaajili ya kutetea taifa ikiwemo vita ya kagera mwaka 1978.
Mh. Paul Makonda amesema hayo leo Mei 17, 2018 wakati wa alipokuwa
anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha
uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa
alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi
“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu
ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na
mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania”
amesema Makonda
Makonda aliongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi
imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye
changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.
Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha
SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha
Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.
Thursday, May 17, 2018
"Baba yangu Alipigana vita ya Kagera" - Makonda
Related Posts:
Mbowe: Tutakata Rufaa hata kama Sugu ameachiwa Huru Kufuatia kuachiwa huru kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga kutoka Gereza la Ruanda, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema bado hawajaf… Read More
BREAKING: Sugu na Masonga Waachiwa Huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya ku… Read More
Sugu Azungumza Baada ya Kuachiwa Kutoka Gerezani Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, am… Read More
Mbunge CCM Adai Kugawana Miradi ‘kimjomba Mjomba’ Kumewakosesha Maji Wananchi Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Mohamed Kessy amesema anao ushahidi wa baadhi ya viongozi wakubwa waliomilikishwa miradi ya maji katika Mkoa wa Rukwa namna wanavyomshawishi ili asizungumze kuhusu ubadhirifu uliopo … Read More
Mbowe Atua Mbeya Kuongoza mapokezi ya Sugu anayetoka jela Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho wamefika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Ka… Read More
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment