Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amemteua Naibu Kamishna wa
Polisi, Maulid Makabila kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (D/DCI)
Zanzibar, huku akifanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa polisi wa
mikoa.
Kabla ya uteuzi huo, Makabila alikuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia uhalifu makao makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi Mei 17, 2018 na msemaji wa polisi, Barnabas
Mwakalukwa imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo aliyekuwa DCI Zanzibar,
Ramadhan Ng’anzi ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
kuchukua nafasi ya Charles Mkumbo aliyehamishiwa makao makuu ya
upelelezi, Dar es Salaam.
Aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa
Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali anakwenda kuwa kamanda wa polisi Mkoa
wa Kaskazini Pemba. Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
polisi, Thobias Sedoyeka aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es
Salaam.
“Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Makarani
Khamisi amehamishiwa makao makuu ya upelelezi Zanzibar na nafasi yake
kuchukuliwa na kamishna msaidizi wa polisi, Suleiman Hassan aliyekuwa
mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kaskazini Unguja,” anasema Mwakalukwa katika
taarifa hiyo.
Aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Hasina Ramadhani Taufiq anakuwa ofisa mnadhimu makao makuu ya
polisi Zanzibar na nafasi yake inachukuliwa na kamishna msaidizi, Haji
Abdallah Haji aliyekuwa ofisa mnadhimu Mkoa wa Mjini Magharibi.
Taarifa hiyo inaeleza mabadiliko hayo ni ya kawaida yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Chanzo- Mwananchi
Friday, May 18, 2018
IGP Sirro afanya mabadiliko Polisi
Related Posts:
Serikali Yasisitiza Nchi iko Salama SERIKALI imewatoa hofu Watanzania wote Bara na Visiwani kuwa nchi iko salama na inaendelea kuwa salama pamoja na kuwapo kwa vitisho kwa njia ya mtandao. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya … Read More
Kujitoa EU: Uingereza Yawatoa hofu Watanzania Siku chache baada ya Uingereza kuamua kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), Balozi wa nchi hiyo nchini amesema wataendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania ili kuhakikisha uwekezaji haupungui. Akijibu swali kuhusu ath… Read More
Waziri wa Afya asitisha zoezi la utoaji chakula Hospitali ya Taifa Muhimbili Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesitisha zoezi la utoaji chakula kwa wagonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka hapo serikali itakapojiridhisha faida na hasara ya zoezi hilo. Hii ndio Tanzania. ------------------------… Read More
TANZIA: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo afariki dunia Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kilindi mkoani Tanga, ndugu Beatrice Shelukindo amefariki dunia Leo jioni jijini Arusha alikokuwa akijiuguza. Mwili umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mount Meru.… Read More
Gesi ya Helium ya Futi za ujazo B ilioni 54 Yagundulika Tanzania GESI ya helium ya takribani futi za ujazo bilioni 54 inayoelezwa kuwa adimu duniani, imegundulika nchini Tanzania na kuiweka nchi kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye madini mengi na muhimu. Wagunduzi wa gesi … Read More
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment