Home »
SIASA
» Profesa Mwandosya: "Hongera Sugu umehitimu chuo cha uanasiasa gerezani"
Waziri
wa serikali ya awamu ya nne Prof. Mark Mwandosya ameingia katika
Orodha ya watu walioonesha furaha yao baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi kuachiliwa jana kutoka gerezani ambapo alihukumiwa
kifungo cha miezi mitano.
Prof. Mwandosya ameandika katika ukurasa wake wa twitter; “Nikimpa
hongera Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha
Uanasiasa, gereza la Ruanda, Mbeya. Kutofautiana vyama, itikadi na
misimamo kusilete uhasama na uadui. Mungu Ibariki Tanzania.”
0 comments:
Post a Comment