Muigizaji
wa Bongo movie Irene Uwoya amesema tangu rafiki yake Agnes Gerald
‘Masogange’ atangulie mbele ya haki amekuwa akihofia kutokewa na mzuka
wake.
Uwoya
ambaye alikuwa na ukaribu mkubwa na rafiki yake marehemu Msasogange
amekiri kuwa tangu msiba huo amekuwa na hofu hata ya kukaa mwenyewe.
Kwenye
mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Global Publishers , Uwoya
alisema, kwa jinsi walivyokuwa karibu na Masogange, amekuwa akiwaza
mengi na ndiyo maana ameshindwa kabisa kuishi katika nyumba ile
waliyokuwa wanaishi jirani na mrembo huyo, maeneo ya Makongo Juu jijini
Dar.
"Nahofia kweli jamani kutokewa na Masogange. Kwa sasa imenibidi niwe mtu wa kujichanganya sana ili nisiwe namkumbuka Masogange”.
Masogange
aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya Kuugua na kulazwa katika
hospitali ya Mama Ngoma na kisha baadae kuzikwa kijijini kwao Mbeya.
0 comments:
Post a Comment