Msanii
wa Bongo muvi nchini, Wema Isaack Sepetu amesema amejiwekea mipaka na
mwanamitindo Hamisa Mobeto kwani amesema mazoea yakizidi sana na
mlimbwende huyo hupelekea mushkeri.
Wema
amesema hayo pindi alipoulizwa juu ya uhusiano wake na mlimbwende
Hamissa Mobeto mara baada ya kuzaa na aliyewahi kuwa mpenzi wake,
Diamond Platinumz na kujikuta anapunguza urafiki waliokuwa nao hapo
awali.
”Hamisa
ni kama Mdogo wangu, lakini kuna wakati sijui mazoea yakizidi sana
kunaleta mushkeri kidogo, kwahiyo kila mtu anatakiwa kubaki kwenye
mipaka yake,” amesema Wema.
Amezungumza
hayo katika hafla fupi iliyoandaliwa na wasanii wa Bongo muvi ya
kumpongeza mwanadada huyo kwa kujishindia tuzo za Sinema Zetu
zilizoandaliwa na Azam Tv mwezi uliopita.
Aidha,
Wema aliwashukuru wasanii wenzake kwa hafla hiyo na kusema ameyasikia
maneno ya baadhi ya wasanii walioponda baada ya yeye kupata tuzo hizo,
lakini anazichukulia kama changamoto za kimaisha.
Azam
Tv ilitoa tuzo hizo usiku wa Pasaka, Aprili 1, 2018 ambapo Wema Sepetu
alishinda tuzo mbili ambazo ni tuzo ya ”Best Views Choice” yaani tuzo
iliyopendekezwa na mashabiki na sio majaji, na Tuzo nyingine ni
Muigizaji bora wa kike.
0 comments:
Post a Comment