test

Monday, February 13, 2023

TAMASHA LA LADY IN RED YAFANYIKA JIJINI DAR

 

TAMASHA la ''Lady in Red'' lafanyika Dar wabunifu na wanamitindo chipukizi wapatiwa tuzo kama pongezi ya Sekta ya ubunifu na wanamitindo kutambua mchango wao.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Hugo Domingo, Mario Frenandes akizungumza wakati wa tamasha hilo amesema kuwa waandaji wa onyesho hilo kwa Msimu wa pili  wa "Lady in Red limekuwa moja ya jukwaa linalotoa fursa mbalimbali sekta ya ubunifu,wanamitindo, mapambano na Muziki.

"Huu ni msimu wa pili tunaendelea kuunga mkono jukwaa hili lengo ni kuwapa nafasi wenye vipaji kuonekana katika sekta mbalimbali na ndio hasa lengo la Hugo Domingo kuona vijana wanafanya kazi kutokana na ujuzi wao na hata kwenye Tamasha hili hatukubagua tumeshirikiana nao wanamuziki,washereheshaji na wasanii.

Fernandes amesema Tamasha hilo kwa mwakani wanatarajia kufalifanya kwa ukubwa sana na kushirikisha wabunifu kutoka nje huku Tamasha likitarajiwa kufanyika Visiwani zanzibar.

Ameeleza namna jukwaa hilo kwa mwaka huu kutimiza kwake miaka 20 tangu kuasisiwa na Mbunifu Mkongwe Mama Asia Khamsin imepelekea wao kama waandaaji wa jukwaa hilo kwa utofauti na kwa ukubwa zaidi .

"Mitindo sasa hivi inafanya vizuri mwakani tuna mpango wa kuanza visiwani Zanzibar na kilele chake kumalizika Dar es Salaam, hivyo wabunifu wajiandae kuonyesha mavazi yenye viwango vya juu zaidi."
Pia ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa sekta ya Mitindo wa endelee kuunga mkono Tamasha hilo ili liendelee kuwepo kila mwaka kwa lengo la kuwaunga mkono wabunifu chipukizi pamoja na wanamitindo.

Katika Tamasha hilo liliweza kutoa tuzo ya Heshima kwa Muasisi wa tamasha hilo Mama Asia Khamsin kwa kutoa vipaji vingi ambavyo kwa sasa ni wabunifu wakubwa Afrika akiwemo Ally Remtullah,Noel stylish pamoja na wengine mbalimbali.

Tamasha hilo ni miaka 20, onyesho la mitindo la Lady In Red limetumika kama jukwaa la kizazi kipya cha mitindo, Lady in Red imeanzishwa na Asya Idarous Khamsin mnamo mwaka 2003.

 Maonyesho hayo pia limewakuza wabunifu wa mitindo mbalimbali  kama vile  Ally Rhemtula, Miriam Odemba, Khadija Mwanamboka, Mustafa Hassanali, Martin Kadinda, Flaviana Matata, Ria Fernandes, Victoria Martin na wengine wengi. 
 
Miaka ya hivi karibuni Asya Idarous alianzisha ushirikiano na kampuni ya Hugo Domingo Limited, kampuni maarufu ya upambaji yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ikiwa na Ofisi pia Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar na ikiwa na Mahusiano pia na nchi mbalimbali za Afrika.







0 comments:

Post a Comment

TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU