Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatibu (CCM) ameiomba serikali kukifuta Chama cha Wananchi (CUF) kutokana na kuhusika na vurugu Pemba.
Akijibu
swali la Munira kuhusu kufuta chama cha CUF kwa madai kuwa kinachochea
machafuko hayo, Naibu Waziri alisema jambo hilo liko mikononi mwa
Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye anatakiwa kuangalia mihemuko hiyo ya
kisiasa.
Swali la Munira lilisababisha Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kuomba Mwongozo na kusema, “Mheshimiwa
Naibu Spika nalazimika kuomba Mwongozo huu, kuna wakati naamini
serikali yetu ikiwajibika kwa pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa
hayumo humu ndani ambaye tunaamini ni sehemu ya serikali.”
Naibu
Spika, Tulia Ackson, alitolea ufafanuzi kuwa kufutiwa usajili kwa CUF
kutatokana na wanachama wake kufanya vitendo visivyofaa na kuathiri
maisha ya watu na mali zao.
Masauni
alisema kuwa maisha ya watu wa Pemba yamekuwa ya hofu wakati wote na
hasa inapotokea kipindi cha uchaguzi kuisha na kusisitiza kuwa serikali
imedhamiria kushughulikia jambo hilo.