Ni
nia ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa mkutano kati yake
na Rais wa Marekani Donald Trump uendelee, imeeleza taarifa ya vyombo
vya habari vya Korea Kaskazini.
Hii ni kutokana na mkutano wa kushtukiza wa siku ya Jumamosi kati ya Kim na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.
Rais
Trump alisitisha mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni
kuzungumzia mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini, lakini alisema Jumamosi
kuwa mambo yanaendelea vizuri sana
Wakati huo huo ujumbe wa Marekani uliripotiwa kwenda Korea Kaskazini siku ya Jumapili.
Balozi
wa zamani wa Marekani nchini Korea Kusini, Sung Kim, atafanya
mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini kuhusu
maandalizi ya mkutano, vyombo vya habari vya Marekani na Korea Kusini
vimeeleza.
Mkutano
huo ni matunda ya jitihada za kidiplomasia ambazo zilianza mwaka huu
kujaribu kuondoa hali ya msuguano uliohofiwa kugeuka kuwa makabiliano ya
kijeshi kati ya Korea Kaskazini, Korea Kusini, na Marekani.
Credit:BBC
0 comments:
Post a Comment