Naibu
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo asubuhi ameahirisha Bunge mpaka
kesho saa tatu asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge
wa Buyungu Mwl. Kasuku Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Vilio
na simanzi vilitawala katika ukumbi wa Bunge kutokana na kifo hicho cha
Mbunge huyo wa Chadema aliyefariki dunia Jumamosi Mei 26.
“Waheshimiwa
wabunge, Spika wa Bunge mheshimiwa Job Ndugai anasikitika kuwatangazia
kifo cha mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago kilichotokea juzi katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa mujibu wa kanuni zetu, leo shughuli
za Bunge hazita endelea na badala yake tutakuwa na maombolezo,” amesema
Naibu Spika.
Wakati Naibu Spika Ackson akitoa taarifa za msiba na kuahirisha Bunge, wabunge Julius Kalanga (Monduli), Suzan Kiwanga (Mlimba), Halima Mdee (Kawe) na Dk Semesi Sware (Viti Maalum ) wote wa Chadema walikuwa wakilia.
Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (Chadema) alishindwa kabisa kujizuia na wabunge walilazimika kumpa usaidizi.

Spika Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge watakao kwenda kuwakilisha kwenye
mazishi hayo wataondoka Dodoma siku ya Jumanne asubuhi na kurejea
Dodoma Jumatano mara baada ya mazishi hayo kumalizika.
Pamoja
na hayo, Naibu Spika ameendelea kwa kusema "siku ya kesho tutakuwa na
kikao cha Bunge kama kawaida isipokuwa tutahairisha Bunge saa sita
mchana ili kutoa fursa kwa shughuli za heshima za mwisho kwa mwili wa
marehumu Bilago na baada ya hapo tutaendelea na maombelezo hadi siku ya
Jumatano".
https://saglamproxy.com
ReplyDeletemetin2 proxy
proxy satın al
knight online proxy
mobil proxy satın al
8PC