Mwanadada
Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja amabao kila siku hawaishiwi na
drama katika mitandao wanakuja tena kivingine na kuelezea jinsi mwezi
mtukufu wa Ramadhani unavyodumisha mahusiano katika ndoa yao.
Irene
anasema kuwa akiwa kama mke halali wa Abdul (janjaro) anahaki zote za
kukaa na kutulia kipindi hiki cha ramadhan na kumpikia mume wake kwa
sababu hicho ni kitu alichozoea hata katika ndoa yake iliyopita.
"Kuhusu
kufunga kwa upande wangu nilishazoea kwa sababu hata siku za nyuma za
ramadhani nilikuwa nikifanya hivyo hivyo nilipokuwa na Ndiku na kwa
sababu sasa hiv mimi ni mke halali kabisa wa Abdul basi nina haki ya
kutulia na kumpikia mume wangu futari."-Uwoya
0 comments:
Post a Comment