Mbunge wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la
Sugu, amesema alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka
juu, na kueleza kwamba ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela
Akizungumzia suala hilo Sugu amesema kwamba kitendo hicho kilimshangaza
kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi walikuwa hawana sare na
wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo kitendo cha
kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa kinamshangaza.
“ Nisiite kujisikia vibaya niite kushangaa, ni siku ambayo maagizo
kutoka juu, ilipigwa simu kwamba lazima Sugu avae uniform na Masonga,
unaweza ukaona kwamba zaidi ya wafungwa 600 hawana uniform, Sugu yuko
pale mmemfunga kwa miezi mitano, anatakiwa kutumikia kama miezi mitatu,
lakini unamlazimisha avae uniform, lakini kuna wafungwa pale wamefungwa
maisha mamia kwa mamia hawana uniform, kwa nini usiangalie namna ya
kuwapatia wale uniform unahangaika na mtu ambaye anapita tu!?”, amesema
Sugu.
Sugu ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha yeye kulazimishwa kuvaa
sare hakikumkwaza kwani aliona inamsaidia kuhifadhi nguo zake.
“Zilitafutwa siku hiyo hiyo uniform, wakaja wakatuletea uniform ambazo
zimevaliwa tukagoma, tukakataa kwa sababu hatuwezi kuvaa nguo ambazo
hatujui zimevaliwa na nani, wakaenda kuhangaika kila kona sijui walitoa
Segerea, lakini walitumia nguvu kuhakikisha wanatuvalisha uniform, wao
walidhani wakimvalisha Sugu uniform ataathirika kisaikolojia, lakini we
umeshanifunga kuvaa nguo ni kitu gani, kwanza utanisaidia kutunza nguo
zangu", amesema Sugu.
Sugu aliachiwa huru mapema wiki iliyopita kwa msamaha wa Rais baada ya
kutumikia kwa muda mfupi kifungo chake cha miezi mitano katika gereza la
Ruanda mkoani Mbeya, akiwa na mwenzake Emmanuel Masonga
Thursday, May 17, 2018
Alicholazimishwa Sugu kufanya akiwa gerezani
Related Posts:
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Aandaa Ibada ya Shukrani Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameibuka na kukabidhi ofisi na akatoa ratiba ya shughuli zake katika Jimbo lake la Misungwi ikiwamo ibada ya shukrani.… Read More
Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli Kauli ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi Nchini Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Ra… Read More
Serikali Yakanusha Madai Kuwa Haina Mpango wa Kuwapanga Vijana Waliohitimu Kidato cha Nne kwenda kidato cha Tano Serikali imekanusha madai ya kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa sababu mbalimbali. Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Wazir… Read More
Serikali yakubali yaishe: Bunge kurushwa LIVE Redioni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema serikali imekubali kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja kupitia redio nchini. Hapo Mwanzo, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape… Read More
Magufuli afanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya. Mulongo atemwa, Polepole ahamishiwa Ubungo.. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kija… Read More
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment