TAMASHA
la ''Lady in Red'' lafanyika Dar wabunifu na wanamitindo chipukizi
wapatiwa tuzo kama pongezi ya Sekta ya ubunifu na wanamitindo kutambua
mchango wao.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Hugo Domingo, Mario Frenandes akizungumza wakati wa
tamasha hilo amesema kuwa waandaji wa onyesho hilo kwa Msimu wa pili wa
"Lady in Red limekuwa moja ya jukwaa linalotoa fursa mbalimbali sekta
ya ubunifu,wanamitindo, mapambano na Muziki.
"Huu
ni msimu wa pili tunaendelea kuunga mkono jukwaa hili lengo ni kuwapa
nafasi wenye vipaji kuonekana katika sekta mbalimbali na ndio hasa lengo
la Hugo Domingo kuona vijana wanafanya kazi kutokana na ujuzi wao na
hata kwenye Tamasha hili hatukubagua tumeshirikiana nao
wanamuziki,washereheshaji na wasanii.
Fernandes
amesema Tamasha hilo kwa mwakani wanatarajia kufalifanya kwa ukubwa
sana na kushirikisha wabunifu kutoka nje huku Tamasha likitarajiwa
kufanyika Visiwani zanzibar.
Ameeleza
namna jukwaa hilo kwa mwaka huu kutimiza kwake miaka 20 tangu kuasisiwa
na Mbunifu Mkongwe Mama Asia Khamsin imepelekea wao kama waandaaji wa
jukwaa hilo kwa utofauti na kwa ukubwa zaidi .
"Mitindo
sasa hivi inafanya vizuri mwakani tuna mpango wa kuanza visiwani
Zanzibar na kilele chake kumalizika Dar es Salaam, hivyo wabunifu
wajiandae kuonyesha mavazi yenye viwango vya juu zaidi."
Pia
ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa sekta ya Mitindo wa endelee kuunga
mkono Tamasha hilo ili liendelee kuwepo kila mwaka kwa lengo la kuwaunga
mkono wabunifu chipukizi pamoja na wanamitindo.
Katika
Tamasha hilo liliweza kutoa tuzo ya Heshima kwa Muasisi wa tamasha hilo
Mama Asia Khamsin kwa kutoa vipaji vingi ambavyo kwa sasa ni wabunifu
wakubwa Afrika akiwemo Ally Remtullah,Noel stylish pamoja na wengine
mbalimbali.
Tamasha
hilo ni miaka 20, onyesho la mitindo la Lady In Red limetumika kama
jukwaa la kizazi kipya cha mitindo, Lady in Red imeanzishwa na Asya
Idarous Khamsin mnamo mwaka 2003.
Maonyesho
hayo pia limewakuza wabunifu wa mitindo mbalimbali kama vile Ally
Rhemtula, Miriam Odemba, Khadija Mwanamboka, Mustafa Hassanali, Martin
Kadinda, Flaviana Matata, Ria Fernandes, Victoria Martin na wengine
wengi.
Miaka ya hivi karibuni Asya Idarous
alianzisha ushirikiano na kampuni ya Hugo Domingo Limited, kampuni
maarufu ya upambaji yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ikiwa na
Ofisi pia Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar na ikiwa na Mahusiano pia na
nchi mbalimbali za Afrika.