Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts
Monday, July 11, 2016
Sunday, July 10, 2016
Wasimamishwa kazi baada ya mama kujifungua kwenye korido
Siku
chache baada ya vyombo vya habari kuripoti mjamzito kujifungulia
kwenye korido ya Kituo cha Afya Lyabukande, Shinyanga kwa kukosa huduma,
uongozi wa Halmashauri ya Shinyanga umewasimamisha kazi watumishi
wawili wa kituo hicho kwa tuhuma za uzembe.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba ambaye kwa sasa
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, jana aliwataja
waliosimamishwa kuwa ni pamoja na muuguzi msaidizi wa kituo hicho, Zulfa
Mussa na mhudumu katika maabara, Peter Mazengo.
Kibamba
alisema wamewasimamisha kazi na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka maadili
ya utumishi huku wakipewa siku 14 kujibu kwa utaratibu wa ajira ya
utumishi.
“Baada ya hapo tunasubiri baraza la madiwani ndilo litatoa uamuzi juu yao.”
Alisema
wakati tukio hilo linatokea, watumishi hao walikuwa zamu na kushindwa
kumsaidia mjamzito huyo na kitendo hicho kilibainika kuwa cha makusudi
na uzembe wa wazi.
“Awamu
hii ya tano ni awamu nyepesi kwa kufanya kazi sababu imenyooka na iko
wazi. Mtu anayeona hawezi kwenda na kasi atupishe ili wabaki wanaoweza
kutekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi
na nilishasema mara kwa mara suala hili,” alisema Kibamba.
Kamati
iliyoteuliwa kuchunguza jambo hilo, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga, Dk Athuman Pembe ilibaini kuwa baada ya mjamzito huyo
kujifungua kwenye korido, watumishi ambao hawakuwapo bali walipata
taarifa na kufika kumhudumia mtoto ambaye ana afya nzuri na baada ya
muda aliruhusiwa kurudi nyumbani.
Ilivyotokea
Tukio
la mjamzito huo, Margareth Charles (22), mkazi wa Kijiji cha Kizungungu
lilitokea Julai 2 baada ya kuelezwa na mtaalamu wa maabara kuwa hakuna
huduma waende sehemu nyingine, lakini mama huyo alishindwa kutokana na
uchungu.
Mtendaji
wa Kata ya Lyabukande, Julius Lugende alisema wananchi wamekuwa
wakikilalamikia kituo hicho kwa muda mrefu na ilifikia wakati
waliandamana kuwakataa watumishi waliopo kutokana na wajawazito
kunyanyasika na kujifungua bila usaidizi.
HIZI NDIZO SABABU 10 ZA KIAFYA ZITAKAZO KUFANYA ULE MAEMBE KILA SIKU,SOMA HAPA NIKUJUZE
vingi sana vitakavyokusaidia kiafya.Kupunguza uzito,kuongeza kinga ya mwili wako,na mambo mengi ya
urembo kwa wakina dada na wakina kaka pia,kuna sababu lukuki zitakazo kufanya ule maembe kila siku
CHATI ZA KIAFYA KWA ASILIMIA
105 ZA KALORI
76 ZA VITAMINI C
25 ZA VITAMINI A
11 ZA VITAMINI B6 NA VITAMINI B NYINGINEZO
9 NYUZINYUZI
9 SHABA
7 POTASIAMU
4 MAGNESIAMU
FAIDA ZA KULA EMBE KILA SIKU NI HIZI
1.KUONGEZA UWEZO WA KUONA
Hii ni kwa sababu ina vitamini A za kutosha kukusasidia katika macho yako
2.INATIBU UGONJWA WA ANAEMIA
3.INASAIDIA KUKUKINGA NA KANSA
4. MAEMBE YANASAIDIA KUPUNGUZA UZITO
5.YANAONGEZA NGUVU ZA MENO NA FIZI
6.YANASAIDIA KUPUNGUKA MAFUTA KWA KIASI KIKUBWA
7.YANASAIDIA KUSAGA KWA CHAKULA
8.YANASAFISHA NGOZI YA USO KWA KIASI KIZURI SANA KWA KUPAKA KATIKA NGOZI YAKO KWA DAKIKA 15
NA KUOSHA KWA MAJI SAFI
9.INAONGEZA KINGA YA MWILI
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU


