test
Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

Monday, May 28, 2018

Uwoya Aelezea Jinsi Mwezi Mtukufu Unavyodumisha Penzi Lake na Dogo Janja

Mwanadada Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja amabao kila siku hawaishiwi na drama katika  mitandao wanakuja tena kivingine na kuelezea jinsi mwezi mtukufu wa Ramadhani unavyodumisha mahusiano katika ndoa yao.

Irene anasema kuwa akiwa kama mke halali wa Abdul (janjaro) anahaki zote za kukaa na kutulia kipindi hiki cha ramadhan na kumpikia mume wake  kwa sababu hicho ni kitu alichozoea hata katika ndoa yake iliyopita.
 
"Kuhusu kufunga kwa upande wangu nilishazoea kwa sababu hata siku za nyuma za ramadhani nilikuwa nikifanya hivyo hivyo nilipokuwa na Ndiku na kwa sababu sasa hiv mimi ni mke halali kabisa wa Abdul basi nina haki ya kutulia na kumpikia mume wangu futari."-Uwoya

Thursday, May 24, 2018

Babu Tale Apelekwa mahabusu kwa muda usiojulikana

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemwamuru mkurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections Company Limited, Hamis Shaban Taletale maarufu kwa jina la Babu Tale, kukaa mahabusu katika kituo cha Polisi akisubiri amri ya kupelekwa kifungoni.

Mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Naibu Msajili, Wilbard Mashauri Februari 16, iliamuru Babu Tale na ndugu yake Idd Shaban Taletale wakamatwe na kupelekwa kifungoni baada ya kushindwa kutekeleza hukumu yake.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016, iliwaamuru ndugu hao kumlipa fidia ya Sh250 milioni, Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kwa makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Kutokana na amri hiyo ya kuwakamata, Babu Tale alitiwa mbaroni juzi na jana alipelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya amri ya kumpeleka kifungoni, lakini alilazimika kurudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi kwa kuwa Naibu Msajili aliyetoa amri ya kuwakamata hakuwepo.

Amri hiyo ya kumrejesha rumande ilitolewa na naibu msajili wa mahakama hiyo, Ruth Massam hadi hapo Naibu Msajili Mashauri aliyetoa amri ya kuwafunga atakaporejea kutoka Dodoma alikokwenda kikazi.

Kwa kuwa haijulikani ni lini atarejea, Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Nassib maarufu kama Diamond Platnum, atalazimika kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana mpaka atakaporejea.

Hati ya kuwakamata Babu Tale na ndugu yake ilitolewa April 4, mwaka huu kutokana na maombi ya Sheikh Mbonde kupitia wakili wake Mwesigwa Muhingo.

Sheikh Mbonde aliwasilisha maombi hayo baada ya Babu Tale na nduguye kushindwa kutekeleza hukumu hiyo, yaani kumlipa kiasi hicho walichoamriwa na Mahakama wala kubainisha mali za kampuni yao, au zao binafsi, ili zipigwe mnada kulipia fidia hiyo.

Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde aliieleza Mahakama kuwa Juni 6, 2013 aliingia makubaliano na kampuni hiyo ili irekodi mawaidha yake na kuziuza kisha wagawane faida, lakini baada ya kurekodi masomo saba, walimwambia kuwa walikuwa wameachana na mpango huo.

Alieleza kuwa baadaye alibaini kuwa mikanda ya video ya mfumo wa DVD zenye mawaidha yake zilikuwa zikiuzwa katika mikoa mbalimbali huku zikiwa na majina na namba za simu za wakurugenzi wa kampuni hiyo, ndipo akafungua kesi hiyo.

Baada ya Sheikh Mbonde kuwasilisha maombi ya kuwafunga jela Babu Tale na nduguye, mahakama ilimwelekeza Sheikh Mbonde kuwalipia wafungwa hao watarajiwa pesa za chakula mahakamani na kumtaka pesa kwa ajili ya matumizi mengine kuziwasilisha gerezani.

Kwa mujibu wa Mahakama, gharama za kuwahudumia wafungwa hao wakiwa gerezani ni kama ifuatavyo:

Vifaa ambavyo ni taulo ya kuogea Sh12,000; godoro Sh40,000; mto wa kulalia Sh10,000; chandarua Sh13,000; mashuka manne Sh48,000; kandambili (malapa) Sh3000; mswaki na dawa ya meno Sh2,000 ambazo jumla ni Sh128,000 kwa mtu mmoja na kwa watu wote wawili ni Sh256,000.

Chakula, kifungua kinywa Sh7,000; chakula cha mchana Sh8,000; maji lita tatu 3,000, jumla Sh18,000 kwa mtu mmoja kwa siku na kwa wote wawili ni Sh36,000. Wote kwa mwezi ni Sh1,080,000.

Pia, kuna fedha za tahadhari kiasi cha Sh800,000 kwa kila mfungwa na kwa wote wawili jumla ni Sh1,600,000.

Sheikh Mbonde alisema kuwa tayari ameshawalipia wafungwa hao fedha za chakula ya mwezi mmoja kiasi cha Sh1,080,000 na kusema ataendelea kuwalipia kiasi kama hicho kila mwezi.

Alisema fedha za matumizi mengine kama yalivyoainishwa na mahakama, ziko tayari na kwamba hizo ataziwasilisha kwa uongozi wa gereza baada ya wafungwa hao kufikishwa huko.

Wednesday, May 23, 2018

Mzee wa Upako Ampigia Simu Q-Chief ,Ni Baada ya Kusikia Anaacha Muziki.

Baada ya kuweka wazi dhamira yake ya kuacha muziki, msanii Q Chief amesema amepigiwa simu na watu wengi mmoja wapo ni Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’

Muimbaji huyo amesema kuwa Mzee wa Mpako alionyesha kuguswa na hatua hiyo aliyoamua kuichukua.

“Nimepokea simu kutoka kwa mtu kama Anthony Lusekelo, usiku saa tisa, unaweza kuona ni jinsi gani mchungaji anaweza kuguswa na kusema mwanangu nimetaka kama kulia hivi, nimepigiwa simu na maostadhi wakubwa sana Tanzania hii,” Q Chief ameiambia Clouds TV.

Ameongeza kuwa amefikia maamuzi hayo na hana kinyongo chochote na mtu ila kwa sasa ameona mapenzi makubwa sana kutoka kwa watu kwenda kwa Q Cheif.

Monday, May 21, 2018

Mwanamuziki Barnaba Awakana Wapenzi Wake Wote

Mwalimu na mwanamuziki wa bongo fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yoyote, huku akidai endapo siku ataamua kuweka wazi juu ya mahusiano yake basi watu wafahamu kuwa anaoa ama anamvalisha pete ya uchumba mpenzi wake nasio vinginevyo.


Barnaba ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya picha zake kuzagaa  kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea baadhi ya watu kudai huwenda wanawake hao anatoka nao kimapenzi nasio vinginevyo.

"Sijui chochote kinachoendelea, nilisema siku ambayo nitakuja kumtangaza mwanamke wangu basi kuna mawili naoa au namvisha pete ya uchumba kwa hiyo sina mapenzi ya mitandao sana na mpenzi wangu nimpendae kwa kweli siwezi kumuweka kwenye mitandao, mwanamke wangu ninamuheshimu  na nitakaye kuja kumpa nafasi ya maisha si mwanamke atakayekuja kuwa wa mitandaoni kiukweli sidhani kama mwanamke wangu anatakiwa kuwa kwenye chombo cha maonesho ya mitandao", amesema Barnaba.

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Barnaba tayari ni 'star' na watu wakiniona nipo nimesimama na mwanamke huyu mara yule wanahisi labda ni wapenzi wangu. Mimi sina mwanamke wala mpenzi 'of course am gentleman' muda mwingine nina haja zangu ninajua namna gani ninavyozikidhi lakini sina makubaliano ya aina yeyote ya kimapenzi kama kijana kusema kwamba hapa nimefunga".

Mtazame hapa chini Barnaba akifunguka zaidi.....

Alichokisema Hamisa Mobetto Kuhusu Kupigwa na Mama Diamond

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu taarifa zilizodai kuwa amepigwa na mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Hapo jana katika uzinduzi wa kipindi cha Nyumba ya Imani cha Wasafi TV, Hamisa alipata time ya kuzungumza na waandishi wa habari na kusema jambo hilo ni binafsi zaidi ila kugombana kwa binadamu ni kitu cha kawaida.

“Hilo siwezi kuliongelea, yeah!. is too person, is too private, is too family. Hata vikombe kwenye kabati vinagong’ana, so sisi binadamu vinaweza kutokea,” amesema.

Alipoulizwa iwapo kwa sasa yeye na mama Diamond wana maelewano mazuri, alijibu; ‘Sina kinyongo na mtu, sina bifu na mtu, mimi am just fine, may be yeye mwenyewe sio upande wangu wa kuweza kuelezea,’.

Taarifa za Hamisa kupigwa na mama Diamond zilianza kusambaa Jumatatu ya wiki iliyopita, May 14, 2018 ambapo usiku ya jana yake Hamisa na Diamond walihudhuria katika uzinduzi wa filamu ya Aunt Ezekiel ‘Mama’ na baada ya hapo anadaiwa waliongozana hadi Madale kwa kina Diamond ambapo ndipo kisa hicho kinadaiwa kutokea.

Thursday, May 17, 2018

Steve Nyerere Amchana Mama Kanumba

Muigizaji filamu bongo Steven Nyerere amefunguka juu ya kitendo cha Mama Kanumba kutoridhishwa na kubadilishiwa adhabu Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alifungwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanaye Kanumba.

Steve Nyerere amesema kwamba amefuta namba ya mama Kanumba kwani hana shughuli naye, na asitake kushindana na serikali kwa sababu hata yeye ilimsaidia alipohitaji msaada.

“Mimi namba ya yule mama nimeifuta nimekasirika nimeona hana shughuli tu, kwa sababu anaongea vitu ambavyo havipo yaani, na sikioni kama kina tija.
"Unajua kuna vitu vingine sio vya kukurupuka kuongea, unatakiwa ukae na watu wakupe hata ushauri, halafu yeye sio mtu wa kugombana na serikali, serikali alipokufa Kanumba ilimsaidia sana, hata hapo alipokuwa anaishi ni serikali ilimpa, yeye hakutakiwa kujibu chochote, alitakiwa kunyamaza na maisha yakaendelea.
"Hata ukimfunga Lulu miaka mia, mtoto atarudi!? Sasa usiilazimishe jamii ikuone umefeli na usiilazimishe jamii ikuone una roho mbaya”, amesema Steve Nyerere.

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba mama huyo hapaswi kulalamika sana kwani hana uhakika kama kweli aliua, kwani pia wawili hao walikuwa kwenye mahusiano.

Hongera Hamisa Kwa Kumpendezesha Aunty Ezekiel

Kupitia mobetostyle kwa Mara ya kwanza mbongo muvi aunty Ezekiel alipendeza sana kwa vazi La heshima alilovaa kwenye uzinduzi wa film yake inayoitwa MAMA ktk ukumbi wa Mlimani City, kwa kweli umejitahidi mnoo!



Aunty alipendeza haswaa akanoga,akaonogeka katika siku yake adhimu.

Hongera sana kwa kufungua kiwanda cha ushonaji(Tanzania ya viwanda)naona unapiga hatua kubwa sanaa kimaendeleo na nimeona pia umevalisha mamiss ifm 2018,ni jambo zuri wadada wa wadogo kama wewe ambao mko chini ya miaka 30 mkifanya jitihada za kimaendeleo kama hizo.

hamisamobetto_BizPjA8HkzS.jpg

Hongera sana kwa wadada wa bongo movie pia kwa kuweza kuamua kujishughulisha na biashara tofauti tofauti na kusapotiana katika kazi zenu.

Nimekupenda bure we mdada na Mungu abariki kazi halali ya mikono yako!!
SIGNATURE
One step at a time!

Seebait.com 2018SeeBait Hili Hapa Ndinga Jipya la Diamond Platnumz Toyota Land Cruiser 200 Series 2018

Katika ukurasa wa instagram wa tttrautouprades , wabunifu na waongeza vionjo vya shape za magari makali wameonyesha ndinga jipya la Diamond Platnumz

Wednesday, May 16, 2018

Gigy Money Naye apata dili la ubalozi wa kondomu

Mwanamuziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Gifty Stanford maarufu kama Gigy Money amebahatika kupata dili nono la kuwa balozi wa Kondomu.

Baada ya Amber Lulu kutangaza wiki iliyopita kuwa amekuwa balozi rasmi wa Kondomu hatimaye na Gigy Mahoney amekuwa msanii wa pili kupata dili hilo.

Gigy Money alitangaza habari njema hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

"BALOZI WA BULL CONDOM (Jamani sahivi kwichi kwichi zangu zote natumia Kondomu mpaka Myrah akue)”.

Kwa upande wa gigy Money Dili hili limekuja katika wakati muafaka kabisa kwa sababu ndio kwanza amaetoka kujifungua hivyo ni wakati wake wa kusaka pesa.

Ali Kiba Awatupia Dongo Wasanii Wanaonunua ‘Views’ Youtube

Msanii wa BongoFleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba maarufu kama King Kiba amefunguka na kudai yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika 'views' za Youtube kama baadhi yao wanavyofikilia vichwani mwao.

King Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku kadhaa tokea video yake mpya ya 'Mvumo wa Radi' kushindwa kuendelea kuhesabu idadi ya watu walioitazama jambo ambalo wengi wao walidai kuna  mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha 'views' wengi kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.

"Hii ndio mara ya kwanza kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile. 
"Ila nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi nategemea pesa kutoka 'Youtube views', mimi nafanya muziki najua wapi napata pesa katika muziki wangu. 
"Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na waelewe mimi ni msanii wa aina gani", amesema Alikiba.

Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot katika 'Youtube' ili ionekane watu wana 'view' kwa wingi ila mimi binafsi ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea hata siku moja kwamba Alikiba ameweka 'robot' ili apate 'views' nyingi, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu na kwanini sasa nidanganye watu".

Wimbo wa Alikiba kwa sasa umetazamwa jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia nafasi ya kwanza katika ya video zilizotazamwa kwa kiasi kikubwa kutoka Youtube

Monday, May 14, 2018

Wema Sepetu aeleza sababu za kushindwa kufika kwenye uzinduzi wa filamu ya Aunt Ezekiel

Msanii Kiwango wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza sababu ya kushindwa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu fupi ya dakika 20 ‘MAMA’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika usiku wa jana (Jumapili) Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Madam Sepenga ametoa taarifa hiyo kupitia kwenye mtandao wa Instagram akidai kuwa alichelewa kutokana na Mama yake ndio alimchelewesha na kujikuta ameshindwa kufika kwenye uzinduzi huo.

“I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…😩😩😩,” ameandika Wema kwenye mtandao huo.

Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.

Shamsa Ford : Harmonize Kaniumiza Sana

Muigizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amekiri kuumizwa na kitendo cha Harmonize kumuhusisha mume wake katika ugomvi wake na ex-girl friend wake, Wolper.

Utakumbuka wiki iliyopitia katika kurushiana maneno kati ya Harmonize na Wolper, mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi alitajwa na Harmonize katika orodha ya wanaume 12 aliodai wametoka kimapenzi na Wolper.

Sasa Shamsa amesema si kwa mume wake pekee bali hata mtu wake wa karibu anapozungumzwa kwa ubaya huwa anaumia.

“Lazima uumie ukiwa kama binadamu hasa kwa mtu ambaye unampenda sio lazima kwa mume kwa mtu yeyote ambaye unampenda, yupo katika sehemu ya maisha yako lazima ujisikie vibaya,” amesema Shamsa.

Taarifa Rasmi ya Jeshi la Magereza Kuhusu Lulu Michael Kutoka Gerezani

Taarifa Rasmi ya Jeshi la Magereza Kuhusu Lulu Michael Kutoka Gerezani

Taarifa za muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael”Lulu” kuachiwa huru siku ya leo May 14,2018 zimewafurahisha wengi baada ya kubadilishiwa adhabu na kumalizia adhabu yake nje ya gereza.

Mchekeshaji Steve Nyerere ambaye pia ni msemaji mkuu katika kitengo cha waigizaji (Bongo Movie) ni mmoja wa watu waliofurahishwa na taarifa hizo na kuonesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa instagram.

“Lulu ni jambo la kushukuru sana kwani kila pito naamini Mungu supo pamoja nawe, nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kumshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa msamaha huu naamini umefanya jambo jema sana Rais wangu. Nipongeze mahakama pia na wadau wote mliokuwa mnamuombea mwenzetu kutoka familia njoo Lulu tujenge tasnia yetu sasa”

Babu Seya na Mwanaye Wametaja Sababu za Kushindwa Kwenda Kwao Congo

Wasanii wa muziki wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wameshindwa kwenda nyumbani kwao Congo kwaajili ya shughuli za kimila.

Wawili hao baada ya kusamehewa kifungo chao mwishoni mwaka jana, waliahidi kwenda nyumbani kwao kwa ajili kutembelea kaburi la mama yao mzazi.

Babu Seya amedai hawawezi kwenda nyumbani kwao kwa sasa kwa kuwa bado hawajapata pesa.

“Unajua ukienda nyumbani unatakiwa kuwa na pesa, sisi bado tupo kwenye mihangaiko ya pesa, mambo yakitulia tutaenda,” alisema Babu Seya.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewaomba wadau wa muziki kuidhamini show yake ya kurudi rasmi kwenye muziki baada ya misukosuko ya muda mrefu ya gerezani.

Breaking News: Lulu Michael Yupo Huru......Kabadilishiwa Adhabu na Kupewa Kifungo Cha Nje

Mcheza filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.
 
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu  na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje

Jibu la Hamisa Mobetto kuhusu kufunga ndoa na Diamond

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu iwapo yupo tayari kufunga ndoa Diamond Platnumz mara baada ya muimbaji huyo kuweka wazi atafanya hivyo mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Filamu ya Mama kutoka kwa Aunt Ezekiel, Hamisa alipoulizwa iwapo yupo tayari kuolewa na Diamond alijibu kwa sasa huwezi kuzungumzia hilo.

“Siwezi kujibu hilo swali,” aliongea Hamisa kwa kifupi.

Katika hatua nyingine Hamisa alidai kuwa yeye sio single mother kwani wazazi wenzie wanamsaidia katika malezi ya watoto.

“You can’t call your self Single Mother kama unasaidiwa kulea mtoto na baba watoto wako, so facts is mababa watoto wangu wote wananisaidia kulea watoto vizuri, kwa hiyo siwezi nikasema single mother sababu nasaidiwa kulea watoto,” alisema Hamissa.

Hamisa ni mama wa watoto wawili ambao wa kwanza alizaa na Majay na wapili alizaa na Diamod Platnumz.

Saturday, May 12, 2018

Wema Sepetu Akanusha kuhusu lipstick zake

Mrembo Wema Sepetu amekanushaa taarifa zilidodai kuwa bidhaa zake mpya za lipstick zinafanana na zile za mwanzo.

Wema amesema hilo halina ukweli wowote zaidi ya watu walioamua kuzusha hilo.

“Kiss by Wema sio Wema Sepetu Liquid Matte, Kiss by Wema ilikuwa na mafuta, hii ya pili ni kavu, hazina mafuta and zipo kwenye package tofauti na zina ubora zaidi kuliko zile za mwanzo,” Amesema Wema Sepetu.

September 2017 Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alikanusha taarifa zilizodai kuwa lipstick za ‘Kiss by Wema’ zilipigwa maarufu na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa kueleza kuwa bidhaa hizo hazikuwepo tena sokoni kwa wakati huo.

Ushauri wa January Makamba wampa nguvu Flaviana Matata

Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Bongo, Flaviana Matata ameukumbuka ushauri aliowahi kupewa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba.

Flaviana amesema kuwa kuna kiongozi alimkwaza miaka michache iliyopita alitaka kulipuka akakumbuka ushauri wa waziri huyo aliowahi kumshauri kuwa asishiriki katika mizozo isiyo ya muhimu.

Kuna kiongozi alinikwaza sana miaka michache ilopita nkataka kulipuka nae Ila Kaka yangu @JMakamba akanambia “Choose your battles wisely Mdogo wangu” #ElimikaWikiendi,” ameandika Flavian Matata katika ukurasa wake wa kijamii.

Naye, Makanda alimjibu kwa kuandika “Si unaona heshima yako kwenye jamii bado ipo juu.”

Hata hivyo tofauti na Uana Mitindo Falviana Matata aliwahi kuwa Miss Universe 2007, hivi sasa Mjasiriamali wa bidhaa za kucha ziitwazo Lavy product.
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU