Jeshi
la Magereza nchini limekanusha taarifa zilizoibuliwa na Mbunge wa Mbeya
Joseph Mbilinyi kuhusu kukosekana kwa sare za wafungwa zaidi ya 600,
katika gereza la Ruanda alipokuwa amefungwa.
Msemaji
wa Jeshi hilo Lucas Mboje, amesema kwamba sio kweli kwamba wafungwa
hawana sare na hakuna kitu kama hiko, isipokuwa kuna mahabusu ambao wapo
mule wakiendelea kusubiri kesi zao, na ndio huenda ambao aliwaona bila
sare.
“Hiko
kitu hakipo, halafu asichanganye mambo, kuna mahabusu ambao wao
wanajulikana kwa mujibu wa sheria hawavai sare, sasa asichanganye, mtu
akishafungwa inajulikana lazima avae sare, sasa kuna mahabusu pia, sio
kweli kama kuna tatizo la sare hakuna mtu anakosa sare, hebu fikiria
wafungwa karibia 600 kwenye gereza moja wakose sare ni kitu ambacho
hakiwezekani, hiyo itakuwa ni issue nyingine”, amesema Lucas Mboje.
Mbunge
Joseph Mbilinyi (Sugu) alipotoka jela kwa msamaha wa Rais alisema
kwamba alilazimishwa kuvaa sare za jela wakati kuna watu amewakuta
gerezani zaidi ya mia 6 wamekosa sare na wapo mule ndani.
0 comments:
Post a Comment