Mama
mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa
maarufu kama Mama Kanumba Amelamba shavu zito baada ya kupata mualiko
wa kuenda nchini Burundi.
Mama
Kanumba Amepata mualiko maalumu kutoka kwa wasanii wa filamu wa nchini
Burundi kwa ajili ya kuenda kujifunza kazi za sanaa hasa filamu
wanazofanya.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Mama Kanumba alisema kuwa
baada ya kupata mualiko huo kutokana na wasanii hao kuthamini mchango wa
marehemu mwanaye, ameona ni vyema kwenda na kitu nchini humo ambapo
ataizindua filamu yake inayoitwa Capten Habona.
"Yani
najisikia ni mtu ambaye ninaheshimika ingawa mtoto wangu hayupo hivyo
filamu yangu hiyo nitazindulia huko kwa vile na wao wamenipa heshima
kubwa sana kwa kuwa filamu yenyewe ina historia nzuri sana“.
Mama
Kanumba aliingia Kwenye sanaa miaka michache iliyopita mara baada ya
Steven Kanumba kufariki dunia ambapo alikiri sababu za kimaslahi ndizo
zilizomuingiza Kwenye uigizaji japokuwa mwanaye hakupenda aigize.
0 comments:
Post a Comment