Mbunge
wa Geita Vijijini Joseph Musukuma, amesema kwamba watu wanaomsema Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuhusu watu wasiojulikana na wanao
likashifu jeshi la polisi na kulituhumu kwa mambo yasiyofaa wanalikosea
jeshi hilo, kwani bila wao tusingekuwa salama.
Musukuma
ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na East Africa Television, na
kusema kwamba iwapo jeshi la polisi likiacha kazi kufanya kazi hata kwa
siku moja hakutakuwa na amani, kwani watu watafikia hatua ya kubakana
bila kutongozana.
“Ilitengenezwa
tu chuki kuwa watu wasiojulikana wanatumwa na Makonda, sijui na nani!!
Mara polisi, hii dhana si nzuri, haya matukio yametokea sehemu nyingi,
Kibiti huko, sijui wapi huko, ila mnalichafua tu jeshi la polisi , Siku
jeshi la Polisi likisema liache kufanya kazi, hali itakuwa mbaya,
hatutatongozana tutabakana.”, alisema Musukuma.
Sambamba
na hilo Musukuma amesema watu wanaofanya hivyo hawako sahihi, kwani
badala yake wanapaswa kulishukuru jeshi hilo kwa jukumu la kuwalinda wao
na mali zao.
0 comments:
Post a Comment