WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa wafanyabiashara na wenye
viwanda vya mafuta ya kupikia na sukari nchini kuhakikisha bidhaa hizo
zinaendelea kupatikana katika maeneo yote na katika bei ya kawaida.
“Natoa
siku tatu kuanzia Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi mafuta yote yaliyoko
bohari yaondolewe yaendelee kusambazwa kama kawaida nchini kote ili
kuondoa uhaba uliojitokeza na kamwe Serikali haitokubali kuchezewa na
wafanyabiashara wasiowaaminifu,”
Ametoa
agizo hilo jana jioni (Jumatano, Mei 9, 2018) Bungeni Jijini Dodoma
mara baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles
Mwijage kutoa kauli ya Serikali kuhusu uhaba wa mafuta ya kupikia
nchini.
Alisema
kama uhaba wa bidhaa hiyo utaendelea, ifikapo Jumapili Serikali itaanza
kufanya msako kwenye viwanda na maghala na kuchukua hatua kali kwa
watakaobainika kuficha mafuta hayo.
Waziri
Mkuu amesema takwimu zinathibitisha kwamba mafuta ya kupikia
yaliyoingizwa nchini yanatosha, hivyo nchi haipaswi kuwa na uhaba.
Amesema kwa mwezi mafuta yanayotumika nchini tani 28.9 na kila mwezi
zinaingizwa tani 30,000.
“Hatuwezi
kukubaliana na jambo hili kwa sababu haliko kwa bahati mbaya ni mpango
uliopangwa kwani imekuwa ni kawaida kila tunapoelekea kwenye Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani kunakuwa na upungufu wa bidhaa hasa sukari, hivyo
Serikali haitakubali wananchi wateseke bila sababu za msingi,”
alisisitiza.
Akiwasilisha
kauli ya Serikali Bungeni, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Bw. Mwijage alisema vyanzo vinavyotumika kuzalishia mafuta nchini
vinatosheleza mahitaji kwa asilimia 30, hivyo asilimia 70 ya mafuta
huagizwa kutoka nje ya nchi.
“Miezi
mitatu ya mwanzo kwa mwaka huu kuanzia Januari wastani wa mafuta
yaliyoingizwa ni tani 30,210.71 kwa mwezi na jumla ya akiba ya mafuta
yaliyopo nchini ni wastani wa tani 68, 902, hivyo hakuna upungufu,”
alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Post a Comment