DARESSAL AA M: Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na
Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea
baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul
Juma.
Tukio hilo lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja
maarufu kwa jina la Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar
ambayo baba wa msanii huyo anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata
‘kinywaji’.
Mtoa ubuyu wetu aliyelipigia simu Amani alisema kuwa, warembo hao
walitangulia kufika katika baa hiyo na kupiga stori pamoja huku wakipata
kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika nao, kila
mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake. “Yani walianza kubishana. Ghafla
wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua. Baba Diamond
kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo chetu.
Baada ya kuunasa ubuyu huo, Amani lilimvutia waya baba Diamond ambaye
alishtuka kusikia habari zimetua gazetini na kusema: “Ni kweli lakini
please naomba upotezee maana wale wote sio watu wangu wewe si unajua
mimi nina mke wangu, mambo ya kilabuni hayo babu
Thursday, May 10, 2018
TANGAZA HAPA KWA BEI NAFUU
0 comments:
Post a Comment