Mkazi
mmoja mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa
kusababisha kifo cha mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia
upasuaji wa tezi dume.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia Shabani upasuaji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia Shabani upasuaji.
Alisema
mtuhumiwa huyo anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya
serikalini, lakini baada ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba
ikiwamo ya upasuaji nyumbani kwake kinyume na sheria.
Baada
ya kumfanyia upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu
nyingi na kuwa katika hali mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo,
alimtelekeza na kukimbilia kusikojulikana.
Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.
Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.