Na David John Pwani
MWENYEKITI
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema
anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama
tulii kabisa.
Amesema
kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo
ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi
nakudai kuwa amejisikia furaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.
Amesema
wakati akielekea kutangaza nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake
Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa
kwenye Komputa.
Dkt.Kikwete
aliyasema hayo jana wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha
Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.
Alisema
anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoanzia na kwamba
amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama
Maji kwenye mtungi.
Akikumbuka
mchakato wa mwaka jana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini
mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .
"Ilikuwa
Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye
uchaguzi ambao ulikuwa na vurumai" alisema Dkt.Kikwete .
Aidha
alisema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye
alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi
jirani.
Alisema
kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma
maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule
huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani
pale alipojaribu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo kanakamba wananchi
wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.
Aidha
Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa
barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita,
Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi
kufikia wabunge kulumbana.
Alisema
hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa bahati nzuri
amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku
akitaka watanzania kumuunga mkono.