Marekani
imelaani mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na Iran katika eneo
linalokaliwa na Israeli –Golan Heights na kuwa halikubaliki na ni hatari
kwa maendeleo ya eneo lote la Mashariki ya Kati.
Katika
tamko lililotolewa Alhamisi, Ikulu ya Marekani imesema kuwa walinzi wa
jeshi la Mapinduzi la Kiislam la Iran (IRGC) “litawajibika kikamilifu
kwa matokeo yoyote ya vitendo vyao vya ovyo” na kuonya kuwa jeshi hilo
na “wanamgambo wanaopigana kwa niaba yao” wasiendelee kufanya “vitendo
vya uchokozi zaidi.”
Israel
imesema Alhamisi ndege zake za kivita zilipiga dazeni ya vituo vya
kijeshi vya Iran ndani ya Syria usiku wa Jumatano ikiwa ni hatua ya
kujibu mashambulizi hayo.
Jeshi
la Israeli limesema kuwa shambulizi hilo la anga lililenga vituo vya
kijasusi, maghala ya silaha na vituo vya kupanga vita, na kuwa ndege
hizo za kivita pia ziliangamiza mifumo ya ulinzi wa anga ya Syria.
Pia
Israel imeonya kuwa “haitoruhusu vitisho vya Iran kujikita katika ardhi
ya Syria” na wamesema serikali ya Syria itawajibishwa “kwa kila kitu
kinachotokea katika ardhi yake.”
0 comments:
Post a Comment