Spika
wa Bunge, Job Ndugai amesema kuna haja ya wabunge kuwaombea mawaziri
kwenye mamlaka husika ili wapate fursa kusafiri nje ya nchi.
KauIi
hiyo ya Spika imekuja kufuatia hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto
Kabwe, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara
na Uwekezaji ambapo alisema ni muhimu Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage asafiri nje ya nchi, ili kujenga uhusiano ya
kidiplomasia na kutafuta masoko ya bidhaa za mbaazi, choroko na
giligilani.
Spika
Ndugai ambaye alikiri kukubaliana na mchango wa Zitto Kabwe amesema ni
kweli mawaziri inabidi wasafiri na wabunge wanapaswa kuwaombea kutoka
kwenye mamlaka.
“Waziri
wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazima aende, tumuombee popote
pale kwenye mamlaka lazima asafiri, maana bidhaa zetu tutauza Kongwa,
kuna soko huko?
“Waziri
wa utalii lazima asafiri ‘apige mawingu’ huko na wengine huko, ndiyo
ukweli jamani, sisi wabunge lazima tuwasemee,” amesisitiza Ndugai.
0 comments:
Post a Comment