Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, ameibiwa gari lake na watu
wanaosadikiwa majambazi, nyumbani kwake Toangoma, jijini Dar es Salaam.
Lyaviva
amesema ameshangazwa na wezi hao kupata ujasiri wa kwenda kuiba
nyumbani kwake bila kujali nafasi yake ya uongozi ikiwamo ya
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
”Yaani
hata hawajaogopa kuja kuiba nyumbani kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama na pia kulikuwa na walinzi wawili,’ alisema.
Akizungumzia
tukio hilo, Lyaniva alisema wezi hao waliingia nyumbani kwake usiku wa
kuamkia juzi kwa kukata uzio na walichukua gari aina ya Toyota IST lenye
namba za usajili T 920 DMQ.
“Wakati
wezi hao wanaingia sikuwapo, nilikuwa safari ya kikazi mkoani Dodoma
lakini kulikuwa na watu nyumbani kwangu. Hata walinzi walikuwapo lakini
wamesema hawajasikia,” alisema.
”Ninao
walinzi wawili na wameniambia hawakusikia chochote lakini Kamanda (wa
Polisi Mkoa wa Temeke) analifanyia kazi tukio hilo maana hata mimi
sielewi vizuri. Ijumaa (juzi) nilipoingia nyumbani ndipo nikapatiwa hizo
taarifa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment