Aliyewahi
kuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt.
Wilbroad Slaa ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden amesema
kuwa mjadala wa kuonekana au kutoonekana kwa sh 1.5 trilioni lililoibuka
baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) limetokana na udhaifu wa mfumo uliopo wa upitishaji wa
bajeti.
Ameeleza kuwa hali hiyo inatokana na mfumo wa Bunge ambao unaruhusu wabunge kupitisha bajeti ambayo fedha zake hazipo tayari.
Dkt.
Slaa amefafanua kuwa wabunge wamekuwa wakipitisha bajeti kabla ya fungu
halisi kupatikana, ikiwa ni nadharia inayosubiri fungu hilo kupatikana
kupitia kwa wafadhili au michakato mingine ya ukusanyaji.
“Kama
fedha nyingi zinatumika bila kupitishwa na Bunge kwa sababu ndiyo mfumo
wetu, unawezaje kuhoji fedha hizo zilitumikaje?” Dkt. Slaa anakaririwa
na Mwananchi waliofanya naye mahojiano maalum.
Aliongeza
kuwa kwa kawaida, huwezi kupata takwimu halisi za miradi mikubwa ya
Serikali ndani ya kipindi cha mwaka wa fedha husika kwani miradi hiyo
huwa katika hatua za utekelezaji.
Balozi
Slaa ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisema
kuwa kinachofanyika hivi sasa bungeni, wabunge wengi hawajadili hoja na
badala yake wamekuwa watu wa kufanya ushabiki na kuhitimisha hoja tu.
Alisema
kuwa wakati alipokuwa bungeni, alikuwa anafanya utafiti wa kutosha
kuhusu masuala ya ufisadi na kuhakikisha anapata nyaraka zote husika
kabla ya kuliwasilisha.
“Ndio maana unaona wakati huo niliweza kuwachachafya Mawaziri kwakuwa nilikuwa sikurupuki,” alisema.
Sakata
la sh 1.5 trilioni liliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
na baadaye kujibiwa na Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment