Muigizaji
wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amekiri kuumizwa na kitendo cha Harmonize
kumuhusisha mume wake katika ugomvi wake na ex-girl friend wake, Wolper.
Utakumbuka
wiki iliyopitia katika kurushiana maneno kati ya Harmonize na Wolper,
mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi alitajwa na Harmonize katika orodha ya
wanaume 12 aliodai wametoka kimapenzi na Wolper.
Sasa Shamsa amesema si kwa mume wake pekee bali hata mtu wake wa karibu anapozungumzwa kwa ubaya huwa anaumia.
“Lazima
uumie ukiwa kama binadamu hasa kwa mtu ambaye unampenda sio lazima kwa
mume kwa mtu yeyote ambaye unampenda, yupo katika sehemu ya maisha yako
lazima ujisikie vibaya,” amesema Shamsa.
0 comments:
Post a Comment