Taarifa
za muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael”Lulu” kuachiwa huru siku
ya leo May 14,2018 zimewafurahisha wengi baada ya kubadilishiwa adhabu
na kumalizia adhabu yake nje ya gereza.
Mchekeshaji
Steve Nyerere ambaye pia ni msemaji mkuu katika kitengo cha waigizaji
(Bongo Movie) ni mmoja wa watu waliofurahishwa na taarifa hizo na
kuonesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa instagram.
“Lulu
ni jambo la kushukuru sana kwani kila pito naamini Mungu supo pamoja
nawe, nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kumshukuru Rais John Pombe
Magufuli kwa msamaha huu naamini umefanya jambo jema sana Rais wangu.
Nipongeze mahakama pia na wadau wote mliokuwa mnamuombea mwenzetu kutoka
familia njoo Lulu tujenge tasnia yetu sasa”
0 comments:
Post a Comment