Mbunge
wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), jana alitema cheche
Bungeni akimnyooshea kidole kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.
Lusinde
alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa wabunge wa Chadema,
wakitaka amfikishie taarifa Mwenyekiti wao huyo kwani hawawezi
kumwambia.
Alisema wabunge hao wamemwambia kuwa wao hawapendi kususia vikao lakini wamekuwa wakilazimishwa na Mbowe.
“Mheshimiwa
Naibu Spika, kati ya viongozi madikteta ndani ya nchi hii ni Mbowe
[Freeman], anawatoa wabunge kwa nguvu. Wabunge [wa Chadema]wako hapo
kwenye chai wamenituma mimi nije niwasemee humu ndani,” alisema Lusinde.
“Wameniomba,
wamesema… ‘Lusinde kuna mambo sisi hatuwezi kumwambia Mbowe nenda
ukamwambie’. Tunatumia fursa hii kumwambia Mbowe warudishe wabunge ndani
ya Bunge, usiwanyanyase. Anawapigia simu wakae kwenye chai badala ya
kuingia Bungeni, tabia gani hiyo,” alisisitiza.
Hata
hivyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi alikanusha taarifa
hizo na kueleza kuwa wabunge hao wanaamini kuwa hivi sasa wanaweza
kuwawakilisha wananchi hata wakiwa nje ya Bunge na kwamba hivi sasa
wanaendelea kufanya vikao vyao wakiijadili bajeti ya Serikali ya mwaka
wa fedha 2016/17.
Sugu
alisema kuwa wanaendelea kujadili Bajeti hiyo katika ukumbi wa zamani
wa Pius Msekwa katika eneo hilo la Bunge na kwamba wanajadili pia njia
bora zaidi ya kuwafikishia wananchi.
Akitolea
ufafanuzi maelezo ya Lusinde, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia
alieleza kuwa wabunge wote wa upinzani wanaotoka Bungeni wakati vikao
vya Bunge vikiendelea wanatoka kwa utashi wao na hawalazimishwi kufanya
hivyo.
0 comments:
Post a Comment