WAZIRI
Mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa,
amemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Katika
barua hiyo, Lowassa amehoji hatua ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku
mikutano na maandamano kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini.
Katika
barua yake hiyo ya jana, Lowassa alisema amelazimika kuchukua hatua
hiyo kwa vile wakati agizo hilo la kupiga marufuku mikutano
inatolewa, alikuwa nje ya nchi ingawa alifikisha ujumbe na Watanzania
wenye nia njema wa ndani na nje kuhusu hatua hiyo ya polisi.
“Kwanza
niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka
taratibu za itifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako.
“Ninafanya
hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo
yaliyonisukuma kukufikishia ujumbe huu yana uzito mkubwa na kimsingi
yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa taifa.
“IGP,
siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia
vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanya hivyo kuweka
rekodi sahihi, na kukosoa sababu ulizotoa kuwa nyuma ya agizo lako
hilo,” alisema Lowassa.
Alisema
wakati akiwa anatafakari kwa mshangao agizo hilo na baada ya kurejea
nchini, alipigwa na butwaa zaidi baada ya kusikia Jeshi la Polisi katika
mikoa ya Kanda ya Ziwa, limewazuia viongozi wao taifa wa vyama vya
siasa kufanya mikutano ya hadhara.
“Agizo
hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwa kwa
viongozi hao, akiwamo Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe huko Mwanza hivi
majuzi.
“Katika
matukio hayo yote, polisi mnadai kuwa na taarifa za intelijensia ambazo
zinaonyesha kuwapo uwezekano wa kutokea vurugu kwenye mikutano hiyo
ya hadhara ya vyama vya siasa,” alisema.
Lowassa
alisema madai hayo ya polisi hata IGP Mangu, aliwahi kuyatoa awali
kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe kama njia ya kuminya haki za
msingi za katiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimiza majukumu yao
ya siasa.
“Si
hivyo tu, uzoefu wa historia unakinzana na kwenda kinyume kabisa na
madai hayo, kwa sababu yako matukio mengi ambayo yamethibitisha kwamba
mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamo maandamano na
hata mikutano, imekuwa ikifanyika kwa amani.
“Iko
mifano mingi inayoonyesha kwamba tumefanya shughuli mbalimbali za
siasa kwa maana ya maandamano na mikutano yahadhara kwa amani na pasipo
kuwapo hata ulinzi wa polisi.
“…Mifano
ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupingane na
maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa uhuru wa katiba wa vyama
vya siasa vya upinzani kujumuika, bali kwenda mbali zaidi na kutilia
shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumo iliyojificha nyuma
ya kichaka cha ‘sababu za intelejensia,” alisema.
Alisema
anaandika barua hiyo aliyoiita waraka kwa mkuu huyo wa polisi kwa
dhati kwamba, kilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama
ilitupilia mbali maagizo ya namna hiyo ya polisi kujaribu kuzuia haki ya
katiba ya vyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea
hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment