Rais
John Magufuli amemteua Prof. Ignas Aloys Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka
mitatu kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.
Taarifa
hiyo ilitolewa na Dk. Leonard Chamuriho, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano jana jijini Dar es Salaam.
“Kwa
mujibu wa sheria Na. 17 ya mwaka 2004 ya Mamlaka ya Usimamizi wa
bandari nchini rais Magufuli amemteua Pr. Rubaratuka ambaye alikuwa
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya TPA,” alisema Chamuriho.
Alisema
kuwa Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuzi ameteuwa watu wanane kuwa
wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu.
“Aidha,
Waziri mwenye dhamana ya sekta ya uchukuzi kwa mamlaka aliyopewa kwa
mujibu wa kifungu Na. 6(2) cha sheria Na. 17 ya TPA ameteua watu nane
kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TPA,” amesema.
Alitaja
wajumbe hao na vitengo vyao wakiwemo Jaffeer Mchano kuwa Mkurugenzi wa
Mipango na Huduma wa Tanzania Investment Bank, Deusdedit Conatus Kakoko
kuwa Meneja Miradi Tanroads.
Wengine
ni Malata Pascal, Mkurugenzi Msaidizi, Division of Litigation and
Abritration na Masanja Kungu Kadogosa kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
0 comments:
Post a Comment