Siku
chache baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima
kuwashutumu viongozi wa CCM kwamba wanamipango ya kutomkadhi chama Rais
Dk. John Magufuli, Shirikiho la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu
Tanzania (TAHLISO), limemshukia na kulaani vikali kauli hiyo kwamba ni
yauchochezi.
Akizungumza
jana latika Ofisi za Shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu wa
TAHLISO Siraji Madebe, amesema, Gwajima kama kiongozi wa dini ajitokeze
hadharani kutaja viongozi anaodai walimpigia simu kuelezea mkakati huo
wa kutomkabidhi Chama Dk. Magufuli.
SOMA TAARIFA KAMILI KAMA ILIYOTOLEWA NA TAHLISO
Shirikisho
la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania limeshitushwa na taarifa
za uchochezi zilizotolewa na kiongozi wa dini wa kanisa la Ufufuo na
Uzima hivi karibuni likituhumu viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa na
mipango ya kutokumkabidhi Chama Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania mh. John Joseph Pombe Magufuli.
Sisi
kama Vyuo Vikuu tunalaani vikali sana kauli yenye dalili za uchochezi
zinazotaka kupandikiza chuki miongoni mwa viongozi wetu wa Serikali na
Chama kwa ujumla.
Lakini
kama kiongozi wa dini mwenye hofu ya Mungu tunamtaka ajitokeze kuwataja
hadharani wale waliompigia simu kumuomba awasaidie bila kuwasahau na
wale wanaozunguka mikoani kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo kama
alivyoeleza.
Ndugu
waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine kwa faida ya watanzania
kiongozi huyu angetaka ufafanuzi juu ya jambo hili angewasiliana na
katibu wetu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Abdulrahman Kinana au Naibu
Katibu Mkuu wetu wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Rajab Luhavi badala ya
kwenda kuaminisha waumini na watanzania jambo lisilokuwa na uhakika.
Lakini
ndugu zangu katika maelezo yake alidhihirisha wazi kwamba hakiungi
mkono Chama Cha Mapinduzi na pia hakumuunga mkono mhe. Rais katika
kipindi cha kampeni, hivyo asichukue nafasi hiyo ya kutaka kugombanisha
na kukisambaratisha Chama Chetu.
Tunatoa
rai kwa viongozi na Taasisi za kidini zote nchini kutojihusisha na
masuala ya kisiasa na badala yake kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa
uwepo wao.
Kuhusisha
siasa na dini ni kuchochea uhasama na kupandikiza mbegu za chuki,
vurugu, uchochezi na kuhatarisha uvunjifu wa amani baina ya wananchi,
viongozi na Taifa kwa ujumla.
Hivyo hatuko tayari kuwavumilia watu wote wenye nia ya kutuvurugia amani tuliyo nayo na kutuingiza kwenye migongano ya kidini.
Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja bila kujali tofauti za kisiasa, kidini na kikabila.
Mwisho
tunapenda kuiomba serikali kupitia vyombo vya dola kushughulikia kwa
kina jambo hili na kulichukulia hatua ili kukomesha vitendo vya
uchochezi baina ya watanzania na baina ya viongozi.
0 comments:
Post a Comment