Serikali
imekanusha madai ya kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa
kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa
sababu mbalimbali.
Akiongea
leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amesema kuwa taarifa hizo ni za uvumi na serikali kwa sasa ipo katika
mchakato wa upangaji wa majina hayo na wakati wowote mwisho mwa mwezi
majina yatakuwa yametolewa.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema moja ya sababu za kuchelewa kwa matokeo hayo ni
pamoja na wizara kubadili mfumo wa GPA, kwenda Division hivyo mchakato
huo ndio unafanywa na serikali ili wanafunzi wote wapate madaraja yao na
waweze kupangiwa shule.
Mhe.
Majaliwa amesema suala la upangaji halikuwa kwa kidato cha tano peke
yake bali pia wale wanaokwenda vyuo mbalimbali na kusema kuwa baada ya
kukamilika watatoa majibu yao wiki mbili kabla ili wazazi waweze
kujiandaa kuwapeleka watoto mashuleni.