Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, jana iliahirisha kesi ya mauaji ya mwanahabari, Daud Mwangosi inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa (FFU), Pasificus Simon hadi leo.
Kesi
hiyo iliahirishwa baada ya upande wa Serikali kufunga ushahidi wake.
Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Februari 12, mwaka 2012, leo inaendelea
kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake mbele ya Jaji Paul Kihwelo
anayeisikiliza.
Katika
kesi hiyo ambayo haikuchukua muda mrefu mahakamani hapo jana, mawakili
wa Serikali wakiongozwa na Sandy Hyra na Ladislaus Komanya walisema
wamefunga ushahidi kwa mashahidi wanne wa awali.
Baada
ya wakili wa utetezi, Rwezaura Kaijage kukubaliana na maombi ya upande
wa Serikali kufunga ushahidi wao, Jaji Kihwelo aliiahirisha kesi hiyo
hadi leo.
Awali,
mtuhumiwa Simon alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali
wa polisi ambao hawaruhusi apigwe picha na waandishi wa habari.
Mwangosi
aliuawa kwa kupigwa bomu Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo
Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa
ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).