SHAMBA la mikarafuu , minazi pamoja na mihogo la Waziri asiye na wizara maalumu Zanzibar Said Soud Said limevamiwa na kuhujumiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia june 14 mwaka huu .
Katika
hujuma hizo zilizotokea katika shamba lililoko Mgelema Jimbo la Chonga
Wilaya ya Chake Chake , jumla ya mikarafuu 29 , minazi 16 pamoja na
mashina 250 ya muhogo yamengo’lewa na baadhi ya mengine kufyekwa na kitu
chenye ncha kali .
Katika
tukio hilo mikarafuu michanga 15 imeng’olewa na kutupwa ndani ya
shamba , na mengine 14 iliyokuwa tayari kuzaa imekatwa na kuachwa ndani
ya shamba .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi , Said Soud Said alivitaka vyombo vya
ulinzi na usalama kuhakikisha vinafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini
waliohusika na vitendo hivyo vya kuhujumu mazao makuu ya uchumi wa nchi .
Aidha
alieleza kwamba , baadhi ya wananchi wanalichukulia suala la siasa kama
ni chuki au fitina , na kuwashangaa wanaoendesha humuma hizo kwani
haziwezi kusaidia kutatua changamoto za kisiasa .
“Ni
jambo la akushangaza kuona mikarafuu , minazi pamoja na mihogo
inafanyiwa hujuma namna hii , ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama
kufanya uchunguzi wa kina ili wausika wapatikane na wafikishwe kwenye
vyombo vya sheria ”alisisitiza.
Mkuu
wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza katika eneo
la tukio alisema Serikali imejapanga vyema kukabiliana na vitendo vya
hujuma na kuwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi
kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo hivyo .
Alisema
kwamba Serikali inategemea zao la Karafuu pamoja na minazi kwa ajili ya
kukuza uchumi wake , na kwamba kitendo cha kukatwa kwa mikarafuu sio tu
kwamba kinarudisha nyumba maendeleo ya mwananchi bali pia na Taifa kwa
ujumla .
“Matendo
haya kwa kweli sio kama yanaathari kwa mwenye shamba pekee , bali hta
uchumi wa Nchi unaathirika kwani Serikali inategemea sana zao la karafuu
kupata fedha za kigeni ”alieleza .
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shekhan Mohammed
Shekhan ameahidi kwamba askari wataendesha doria na msako wa kuwasaka
wahusika ili waweze kufikishwa kwenye mahakamani .
Alisema
kwamba katika msako huo , watawatumia askari Shehia , Polisi jamii
pamoja na wananchi wa kawaida na kuongeza kuwa watakaobainika
watachukuliwa hatua hata kama watakuwa nje ya Mkoa huo .
Kwa
hili hatutakuwa na huruma na mtu , tutafanya kazi kwa mujibu wa sheria
na taratibu za jeshi ,pia tutawatumia askari shehia , polisi jamii
pamoja na raia wema abao wamekuwa wakitupa taarifa ”alisisitiza .
Hivyo
Kamanda shekhan amewataka wananchi kutotumia fursa hiyo kutoa taarifa
ambazo sio sahihi na ambazo zinawahusu wananchi wenye chuki binafsi. Na
kwamba jeshi la polisi litazifanyia uchunguzi taarifa hizo kabla ya
kuzichukulia hatua .
Matendo
ya hujuma kwa baadhi ya mali za wananchi yanaendelea kutokea katika
mikoa ya Pemba baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu wa marejeo uliofanyika
machi 20 mwaka 2016 yakihusishwa na itikadi za kisiasa.
0 comments:
Post a Comment