Rais
Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia
wa Iran. Ameuita mpango huo kuwa umeoza na ni kero kwa raia wote wa
Marekani.
Amesema
mpango huo hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila
kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015
chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.
Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake.
Akienda
kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo,Trump amesema
kuwa watarejesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran
kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.
Israel
na Saudi Arabia kwa pamoja wamepongeza hatua hiyo.Vikwazo vipya
vinatarajiwa kuanza dhidi ya Iran ndani miezi mitatu ijayo.
Trump
awali alilalamikia mkataba huo kwamba ulikuwa unaiwekea Iran vikwazo
kwa muda tu na kwamba ilishindwa kusitisha mpango wake wa makombora
0 comments:
Post a Comment