Hayo
yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TCRA, James Kilaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
utekelezaji wa uamuzi wa kuzima simu feki.
Alisema
mafundi wa simu, wanatakiwa kuomba leseni ya kutengeneza simu na kuweka
utaratibu wa kuwaorodhesha wanaoleta simu zao kutengenezwa ili kuepuka
kuwa sehemu ya mtandao wa wizi wa simu.
Akizungumzia
simu feki, Kilaba alisema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa
hazina viwango, zimebaki kuwa ni asilimia 2.96 huku namba tambulishi
ambazo zimenakiliwa zimefika 0.09.
Kilaba
alisema idadi ya namba tambulishi, ambazo hazina kiwango zimepungua
kutoka asilimia 3 kwa mwezi Mei hadi kufikia asilimia 2.96 huku namba
tambulishi zilizonakiliwa zimepungua kutoka asilimia 2 hadi 0.09.
Alisema
idadi ya namba tambulishi za simu halisi, imeongezeka kutoka asilimia
85 mwezi Mei mwaka huu hadi kufikia asilimia 96.95 ilipofika juzi.
Wakati
TCRA inazindua mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya
mawasiliano vya mkononi Desemba mwaka 2015, idadi ya namba tambulishi
ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zilikuwa sawa na asilimia 4 na
zile ambazo zilikuwa zimenakiliwa zilikuwa ni sawa na asilimia 30.
“Pamoja
na kuwapo idadi ndogo ya watu ambao wanatumia simu feki, msimamo wetu
bado uko palepale ifikapo kesho (leo) saa sita usiku, maana suala la
usalama halitegemei idadi ndogo ya simu hizo,” alisema.
Aliwakumbusha
Watanzania wote kuwa ni jukumu la kila mmoja, kuhakikisha kuwa simu
yake ni halisi na sio bandia, kwani kuanzia leo, hakuna simu bandia
itakayoweza kufanya kazi nchini.
“Nawakumbusha
wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kutambua kuwa ni kosa
kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mkononi, kwani adhabu
yake ni kifungo kisichozidi miaka kumi (10) au faini isiyopungua Sh
millioni 30 au vyote kwa pamoja."
Kilaba
aliwataka wanaofanya biashara za kuingiza simu hapa nchini kutoka nje,
wahakikishe kuwa simu wanazoleta zinakidhi viwango, zimehakikiwa kwa
mujibu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kuwa na leseni ya Mamlaka
ya Mawasiliano kwa mujibu wa Sheria.
0 comments:
Post a Comment