Waendesha
mashtaka wa serikali Morogoro wamepewa miezi miwili kuwasilisha cheti
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kuachia ama kuendelea
kushikilia dhamana ya washtakiwa wanne wa kesi ya usambazaji wa picha
chafu za ngono.
Washtakiwa hao ni wale waliopiga picha chafu za ngono dhidi ya mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Dakawa, Mvomero.
Mbele
ya waendesha mashtaka wa serikali Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki
na Calistus Kapinga ilidaiwa mahakamani hapo na Ivan Msacky, Hakimu wa
Mahakama hiyo kuwa, suala la dhamana chini ya Katiba ni haki ya kila
mshtakiwa lakini akaonesha kushangazwa na upande wa mashtaka kutoeleza
kwa uwazi sababu za kuendelea kuizuia dhamana hiyo.
Hakimu
Msacky amewataka waendesha mashtaka hao kuhakikisha wanawasilisha
mahakamani cheti kinachozuia dhamana kwa washtakiwa hao na sababu zake
ili kesi hiyo iweze kuanza kusikilizwa.
Kesi
hiyo ya jinai namba 54 ya mwaka 2016 inawakabili washtakiwa sita ambao
ni Idd Adam Mabela, Zuberi Thabit, Rajab Salehe, Ramadhani Ally, Muksin
Ng’ahy na John Peter ambao wanakabiliwa na shtaka la kusambaza picha
chafu za ngono za msichana mwenye umri wa miaka 21 wilayani Mvomero
mkoani humo. Washtakiwa wanaotaka dhamana ni mshtakiwa namba tatu hadi
sita.
Hata
hivyo, Hakimu Msacky jana aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 29 Juni
mwaka huu ambapo kesi hiyo itaendelea kujadili suala la dhamana kwa
washtakiwa hao.
Katika
kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 18 Mei mshtakiwa
namba 1 na 2 wanatuhumiwa kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile
msichana huyo Aprili 27, saa 1 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya
TITII iliyopo katika Tarafa ya Dakawa, Mvomero.
Katika
kesi ya kwanza ya kubaka na kulawiti inayowakabili washtakiwa Mabela na
Thabiti, wakazi wa jijini Mbeya ilishindwa kusikilizwa jana kutokana
na wakili wa washtakiwa Mohamed Mkali kutokuwepo mahakamani.
0 comments:
Post a Comment