RAIS
John Magufuli amesema wakurugenzi watendaji (DED) wa halmashauri za
wilaya, miji, manispaa na majiji aliowateua hivi karibuni, hakuwachagua
kwa kubahatisha wala hakuchagua vilaza.
Pamoja na hayo, Magufuli ametoboa siri ya kuihamishia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) chini ya Ofisi ya Rais kuwa ni baada ya kubaini miaka ya nyuma nafasi za ukurugenzi zilikuwa zinatolewa kwa ushawishi na rushwa.
Rais
alisema hayo Ikulu Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya viongozi hao
wapya ya kula kiapo cha Uadilifu wa Uongozi wa Umma kupitia
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kupatiwa semina ya
maadili ya viongozi wa umma.
Alisema
tangu awateue wakurugenzi hao kumekuwa na maneno ya chinichini na
mitandao ya kijamii, ikidai kuwa wengi wao hawana sifa na kufikia hatua
ya kumtaja Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Wilaya ya Itigi mkoani Singida,
Pius Shija Luhende kuwa ni mhudumu wa hoteli iliyopo Sinza jijini Dar es
Salaam.
Ma-DED wana sifa za kutosha
“Lengo
la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwatumikia wananchi na kutimiza ahadi
pamoja na Ilani ya CCM ya mwaka 2015 kwa kipindi cha miaka mitano.
Tayari hadi sasa miezi minane imeshapotea, nataka utekelezaji wa ahadi
hizi uende kwa kasi ya ajabu…
“…Sasa kwa kasi hii ninayoitaka siwezi kubahatisha katika uteuzi wa viongozi watakaofanikisha azma hii. Hawa wakurugenzi niliowachagua asilimia 80 wana Shahada ya Uzamili na wengine wana Shahada na uzoefu wa kutosha,” alisisitiza Rais Magufuli.
“…Sasa kwa kasi hii ninayoitaka siwezi kubahatisha katika uteuzi wa viongozi watakaofanikisha azma hii. Hawa wakurugenzi niliowachagua asilimia 80 wana Shahada ya Uzamili na wengine wana Shahada na uzoefu wa kutosha,” alisisitiza Rais Magufuli.
Kuhusu
uteuzi wa Shija, alisema anafahamu kuwa mkurugenzi huyo ana sifa za
kutosha kuitumikia nafasi hiyo kwa kuwa ana Shahada ya Uzamili na
Stashahada na alikuwa ni mkaguzi wa shule.
“Unajua
baada ya hili la mitandao ya kijamii nimejifunza mengi, ukiona adui
anakushangilia ukifanya jambo, rudi nyuma ujiulize umekosea wapi lakini
ukiona adui yako anakushambulia basi ujue umemtwanga,” alisema Rais Magufuli.
Alisema
anafahamu kuwa nafasi ya ukurugenzi wa halmashauri ni muhimu katika
kujenga uchumi hasa wa chini ndio maana katika kuwateua viongozi hao,
ametumia takribani miezi minne kuwachuja na kuwachambua ili kupata
viongozi wenye sifa na vigezo stahili.
Hongo kupata u-DED
Alisema
zamani wakurugenzi wengi walikuwa wakipata nafasi hiyo kwa kufanya
ushawishi kwa kushirikiana na maofisa wa Tamisemi na kuwahonga fedha.
“Pale
Tamisemi kulikuwa na timu imejipanga kufanikisha hili. Nimeshaagiza
waziri ahakikishe watu wote waliohusika kwa hili wanaondolewa ndio maana
niliamua wizara hii iwe chini yangu kwa makusudi,” alifafanua.
Akizungumzia
uwajibikaji wa wakurugenzi hao, alisema fedha nyingi za serikali
hupelekwa kwenye halmashauri, eneo ambalo limekuwa na sifa mbaya ya
fedha hizo kutumika hovyo bila kuzingatia weledi na maadili.
Alisema
ndio maana katika uteuzi wa wakurugenzi hao kati ya wakurugenzi 185
waliokuwapo, wa zamani walioendelea ni 60 pekee na 120 ‘wametemwa’, hali
inayodhihirisha kuwa waliobaki ni watendaji wazuri ambapo yeye aliwaita
‘majembe’.
Alisema kila mkurugenzi aliyechaguliwa, atambue kuwa sifa zake zilichambuliwa na Rais mwenyewe. “Ndio
maana mimi sitembei, nilikuwa nalala saa sita hadi saa nane usiku,
nawafahamu wote kwa sifa hadi majina, ninaamini hawataniangusha,” alisema.
Aliwataka
kuhakikisha wanazisimamia vyema fedha za serikali zinazowasilishwa
katika halmashauri na kuepuka kuburuzwa, kujipendekeza, kukejeliwa au
kutumika vibaya kwa kuingia mikataba na kampuni feki zisizoweza
kutekeleza vyema wajibu wake.
Fedha za Mfuko wa Barabara
Magufuli
alisema anazo taarifa za baadhi ya wakurugenzi, walikuwa wakishirikiana
na mameya, madiwani na wenyeviti wa halmashauri kwa kupitisha na
kuingia mikataba na kampuni zilizo na uwezo chini ya viwango katika
kutekeleza miradi ya barabara; na matokeo yake miradi mingi haikuwa na
mafanikio.
“Nawaambieni
mkisimamia maadili hakuna atakayewafukuza kazi. Msijipendekeze kwa mtu
kwa sababu hakuna aliyepenyeza majina yenu kwangu hadi mkachaguliwa.
Kuna mmoja jina lake lilipenyezwa nikalitupilia mbali,” alisema.
Fedha za elimu bure
Aliwataka
kuwa makini na kusimamia vyema Sh bilioni 18.77 zinazotolewa na
serikali kila mwezi kwa ajili ya elimu bure katika shule za msingi na
sekondari kwa kuhakikisha zinatumika vyema kwa lengo lililokusudiwa.
Alisema
wapo wakurugenzi waliokuwa wakizitumia vibaya fedha hizo kwa madai kuwa
ni nyingi, huku kukiwa na taarifa za baadhi ya walimu wakuu katika
kufanya udanganyifu kwa kuandika orodha ya uongo ya wanafunzi na
kuongeza idadi ili wapate mgawo mkubwa wa fedha hizo.
Matumizi
ya EFDs serikalini Pamoja na hayo, Rais Magufuli aliziagiza wizara zote
nchini chini ya makatibu wake wakuu na halmashauri za wilaya, miji,
manispaa na majiji na taasisi zote za serikali, kuhakikisha wanaanza
mara moja kukusanya mapato yake kwa kutumia mashine za kielektroniki
(EFDs).
“Haiwezekani
mfanyabiashara alazimishwe kutumia mashine hizi wakati sisi serikalini
tunakusanya mapato yetu bila kutumia mashine za EFDs. Ninawataka nyie
wakurugenzi mliopo hapa mkifika katika maeneo yenu mhakikishe
halmashauri zenu zinakusanya mapato yake kwa kutumia EFDs,” alisisitiza.
Aidha
aliwaagiza wakurugenzi hao kuhakikisha wanashiriki katika kutimiza
ndoto ya Tanzania kuwa taifa lenye kipato cha kati kupitia uchumi wa
viwanda kwa kila mmoja kuhakikisha katika eneo lake kunaanzishwa viwanda
vidogo.
Kodi ndogo ndogo
Akizungumzia
kero na changamoto zinazowakabili wananchi, Dk Magufuli aliwataka
wakurugenzi hao kuhakikisha kipaumbele chao kikubwa kinakuwa ni kuondoa
kero za wananchi hasa wale wenye maisha ya chini.
Alisema
watanzania wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu na kuhangaishwa na kodi
za ajabu hali iliyochangia kurudisha maisha yao nyuma.
“Unakuta
mtu analima mpunga wake, akivuna na kuubeba kuupeleka nyumbani kwa
matumizi anadaiwa kodi, mbona wakati analima hamkudai kodi? “Nawaomba
mhakikishe kodi za aina hii mnazizuia kwani Serikali hii wakati ikiomba
kura ya kuingia madarakani, haikuahidi kutengeneza kero kwa wananchi
bali kuziondoa kero hizo,” alisema.
Kutumbua majipu
Aliwaagiza
wakurugenzi hao watakapofika kwenye vituo vyao vya kazi, kuhakikisha
wanachukulia hatua na kuwaondoa mara moja watendaji walio kwenye mamlaka
yao wasiowajibika na wale wanaofanya kazi kwa kujifanya miungu watu.
“Nina
taarifa wapo watendaji kata ambao wanajifanya miungu watu, kazi yao
kubwa ni kuichonganisha Serikali na wananchi, tumieni madaraka yenu
kuwaondoa ila msimuonee mtu. Nataka mkawe mitume kwa niaba ya Serikali,” alisema.
Magufuli
alisema amewateua viongozi hao kwa kuwaamini na hatarajii itafika siku
atajutia uteuzi wake na kubaini kuwa aliwateua kimakosa.
Makamu wa Rais
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliwataka wakurugenzi
hao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuwa kuhudumia na kusimamia
watumishi wa umma na wananchi; na si kuwa watawala.
“Kila
mtu ajiulize kwa nini Tanzania kwenye watu takribani milioni 50, lakini
ameteuliwa yeye. Someni alama za nyakati na muwatumikie vyema wananchi.
Someni pia mazingira ya kazi, simamieni utendaji wenu kwa misingi ya
sheria na katiba,” alisema Samia.
Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alisema nafasi ya ukurugenzi katika halmashauri
za wilaya, miji, manispaa na majiji ni sawa na injini ya uwajibikaji,
hivyo wanaoshika nafasi hizo wanatakiwa kuwa wachapakazi, waadilifu na
wenye kujituma ili serikali na taifa kwa ujumla lifikie malengo yake.
“Nawataka
mkifika muanze kwanza kuwafahamu vyema washirika wenu kama vile mkuu wa
mkoa, mkuu wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama, sekretarieti ya
mkoa, wakuu wa idara na watumishi. Zijueni vyema ofisi zenu tambueni
maeneo yenu ya kazi,” alisema Majaliwa.
Aidha,
alisema halmashauri pamoja na kuendeshwa kwa fedha za serikali pia zina
vyanzo vyake vya ndani vya mapato na kuwataka viongozi hao kuwa mstari
wa mbele katika kusimamia vyema vyanzo hivyo na ukusanyaji wa mapato
yake.
Aliwataka
kuwa mstari wa mbele kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maagizo ya
Rais likiwemo agizo lake la hivi karibuni la kuhakikisha kila mwanafunzi
wa shule za msingi na sekondari ana dawati.
Ma-DC
Pamoja na wakurugenzi hao kuapa kiapo cha uadilifu, pia wakuu wa wilaya watatu ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu, Agnes Hokororo (Manyoni - Singida) na Miraji Mtaturu (Ikungi – Singida) walikula kiapo hicho.
Pamoja na wakurugenzi hao kuapa kiapo cha uadilifu, pia wakuu wa wilaya watatu ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu, Agnes Hokororo (Manyoni - Singida) na Miraji Mtaturu (Ikungi – Singida) walikula kiapo hicho.
Ma-DC
hao hawakula kiapo cha uadilifu na wenzao hivi karibuni baada ya
kubainika makosa katika uteuzi wa wateule wa awali wa nafasi za wilaya
hizo. Hokororo alichukua nafasi ya aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo
awali, Fatma Toufiq kutenguliwa kwa kuwa tayari ana wadhifa wa ubunge
Viti Maalumu.
Babu
na Mtaturu walichukua nafasi hizo baada ya wateule wa awali ambao ni
Fikiri Avias Said na Emile Ntakamulenga, kutenguliwa uteuzi wao baada ya
kuteuliwa kimakosa.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,
Jaji Salome Kaganda aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanazisoma na
kuzielewa sheria zinazowaongoza ikiwemo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma.
Aidha,
aliwataka kuhakikisha wanatunza maadili yao kama viongozi wa umma na
kutambua kuwa wao na viongozi wa umma kwa saa 24 usiku na mchana hivyo
wajiepushe na masuala yatakayowavunjia heshima na kuwaaibisha mbele ya
jamii.
“Lakini
pia nawahimiza mkumbuke kuwa nyie mtakuwa na siri nyingi za serikali
haitopendeza kumkuta mbunge ana nyaraka zilizoandikwa siri za serikali
kutoka eneo lako. Moja kwa moja utajibu,” alisema.
Jaji
Kaganda alisema amebaini kuwa wateule wengi wa nafasi hizo za
wakurugenzi ni vijana na kuwahimiza kuhakikisha hawaleweshwi na madaraka
hayo na kujiingiza kwenye matendo ya anasa na kujivunjia heshima.