Hakika ni wengi hawakumwelewa lowassa aliposena Chadema iache Mambo ya
uharakati ila wajipange kisiasa kushika dola 2020. Ukweli ni kwamba
Chadema imetumia fedha nyingi kujitangaza, naona wamefanikiwa kujulikana
sana hata kukikosesha amani Chama Tawala ,Sasa ni wakati wa kuweka
mikakati ya kuchukua dola. Chadema ina watu wakubwa ndani ya chama ambao
wanajua mifumo ya nchi kiusalama.
Ni wakati wao wa kufanya mikakati ya kiakili kushika dola.
Kwa nchi za kiafrika kushika dola kwa maandamano ni kujisumbua bure, cha zaidi mtaishiwa kuuwawa na kuteswa tu
Niwakati wa Ukawa kuwa na timu ya strategy isiyozidi kumi, timu yenye
kuaminiana kuhakikisha na wao wanafanya siasa ya kiutu uzima.
Nadhani wakubwa waliopevuka wamenielewaa