Mbunge
wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ameitaka Serikali kuwa na huruma na
watumishi wake iliowaondoa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti feki.
Mdee
ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Mei 23, 2018 wakati
akiuliza swali la nyongeza, kubainisha kuwa kuna watumishi waliotumia
vyeti vya watu wengine kujiendeleza kielimu na wamefanya kazi kwa
uadilifu mkubwa.
Hata
hivyo, Waziri wa Nishati, Angellah Kairuki ambaye wakati wa uhakiki wa
vyeti kwa watumishi wa umma ukianza alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Utumishi na Utawala Bora) amesema hakuna malipo wala huruma yoyote
itakayotolewa kwa wafanyakazi hao.
"
Mdee mdogo wangu na dada yangu wewe ni mwanasheria lazima ujue kuwa
hakuna kitu kama hicho kwa hiyo Serikali haiwezi kuwalipa au kuwapa
msamaha," amesema Kairuki.
Amesema kwa kuzingatia maelezo hayo, mjadala huo utakuwa umefungwa kwani waliostahili kurudi kazini walisharudishwa.
0 comments:
Post a Comment