Iran
imeendelea kupinga masharti kutoka Marekani ya kufanyia mabadiliko sera
yake ya kigeni na mpango wake wa nyuklia huku mshirika wake Syria,
ikitupilia mbali wito wa Marekani kuviondoa vikosi vya Iran nchini humo.
Ufaransa,
mmoja ya mataifa yenye nguvu barani Ulaya, iliosikitishwa na hatua ya
Marekani kujiondoa katika mkataba wa nyuklia uliyotiwa saini mwaka 2015,
imesema hatua ya Marekani ya kuiongezea vikwazo zaidi Iran,
itawaimarisha zaidi wanasiasa wenye msimamo mkali nchini Iran.
Jumatatu
wiki hii waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo
aliitishia iran kuwa itakabiliwa na vikwazo zaidi katika historia iwapo
haitaachana na ushawishi wake wa kikanda, akiishutumu nchi hiyo kuunga
mkono makundi ya silaha katika mataifa kama vile Syria Lebanon na Yemen.
Pompeo
aliyasema haya wiki mbili baada ya rais Trump kujiondoa katika mpango
wa kimataifa wa nyuklia wa Iran, uliopelekea taifa hilo kuondolewa
vikwazo kufuatia hatua yake ya kukubali kusitisha uendelezaji wa mpango
huo.
Mataifa yenye nguvu barani Ulaya yanauona mkataba huo kama nafasi nzuri ya kuizuwia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad Javad Zarif
amesema Pompeo amerejelea shutuma za zamani dhidi ya nchi yake ila
safari hii shutuma hizo zimetolewa kwa ukali zaidi.
Naye
afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Meja jenerali Mohammad Bagheri,
amesema Iran haitaisujudia Marekani katika shinikizo lake la kudhibiti
shughuli zake za kijeshi.
Mjini
Paris, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian
amesema hatua ya Marekani kujiondoa katika mkataba huo wa nyuklia na
kuiwekea Iran vikwazo itazidisha misimamo mikali na kuhatarisha eneo
hilo.
Le
Drian amesema Ufaransa itaendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba huo
hata kama inakubaliana na Marekani kwamba shughuli za nyuklia za Iran
pamoja na makombora zinapaswa kudhibitiwa.
Huku
hayo yakiarifiwa Syria imetupilia mbali wito wa Marekani wa kuviondoa
vikosi vya Iran nchini humo. Katika vita vya Syria vilivyodumu miaka 7,
Iran imekuwa ikitoa msaada muhimu kwa jeshi la serikali ya Bashar al
Assad.
0 comments:
Post a Comment