Bodi
ya Utalii nchini imetoa taarifa kufafanua kuhusu mlima Kilimanjaro
baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa
iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.
Taarifa
hiyo imekuja baada ya kutokea kwa kifo cha dereva wa kimataifa wa mbio
za magari Guguleth Zulu, aliyefariki dunia wakati akipanda Mlima
Kilimanjaro.
Kwa
mujibu wa taarifa ya bodi ya utalii kwa vyombo vya habari imekanusha
taarifa iliyochapishwa na mwandishi wa shirika la AP kwamba milma huo
upo Kenya.
‘’Tungependa kusahihisha habari za kupotosha kwamba mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,”
Aidha Bodi ya Utalii Tanzania imeandika barua kwa chombo cha habari kilichofanya makosa hayo na kutaka wafanye marekebisho.
Miezi
michache iliyopita mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila
Odinga, Rose Mary Odinga akihutubia vijana nchini Marekani aliwaambia
Olduvai Gorge ipo Kenya na baadaye alikanusha taarifa hiyo.